Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba
fupi kwa Wajumbe wa Bodi Mpya ya Shule ya Sekondari Bwawani( hawapo
pichani) kabla ya kuzindua rasmi Bodi hiyo leo Januari 07, 2014 Mkoani
Pwani. 
Mkuu
wa Shule ya Sekondari Bwawani, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Hamza
Rajabu(kushoto) akisoma risala fupi kabla ya kumkaribisha Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja kuzindua rasmi Bodi
Mpya ya Shule ya Sekondari Bwawani leo Januari 07, 2014 Mkoani Pwani.

Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimkabidhi Vitendea
kazi vya Bodi Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Bwawani
ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga mara baada ya
kuzindua rasmi Bodi hiyo ya Shule leo Januari 07, 2014 Mkoani Pwani.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi Mpya ya Shule ya Sekondari Bwawani
mara baada ya kuzindua rasmi Bodi hiyo leo Januari 07, 2014 katika
Ukumbi wa Shule hiyo. Bwawani Sekondari ipo Mkoa wa Pwani. Shule hiyo
ilianzishwa rasmi Mwaka 1978 na ni Shule ya Bweni ikiwa na Mchepuo wa
Biashara na inamilikiwa na Jeshi la Magereza Tanzania Bara(Picha zote na
Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Post a Comment