Mkurugenzi
Mtendaji wa Huduma za Kipolisi wa Interpol Bw. Jean-michel Louboutin
kushoto akimkabidhi Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamdam Omari Makame
nembo maalum ya Interpool,
…………………………………………………..
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
SHIRIKISHO la
Polisi wa Kimataifa Duniani INTERPOL, limesema litaendelea kuunga mkono
juhudi zozote zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha
na kudumisha hali ya usalama wa Visiwa vya Zanzibar kwa lengo la
kuimarisha utalii kwenye eneo hilo.
Ahadi hiyo
imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Kipolisi wa Interpol Bw.
Jean-michel Louboutin, wakati alipokutana na Kamishna wa Polisi Zanzibar
CP Hamdani Omari Makame, aliyetembelea Makao Makuu ya Shirikisho hilo
mjini Lyon Ufaransa ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kiusalama
yanayoigusa Zanzibar kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
Bw. Jean-michel
amesema ipo haja kwa jumuia nyingine za kimataifa kuunga mkono juhudi za
Tanzania katika suala zima la kuimarisha usalama wa eneo hilo lenye
historia inayovuta watalii kutoka katika mataifa mbalimbali.
Katika ziara
hiyo ambayo ililenga kuimarisha usalama wa kikanda, Kamishna Hamdani
alisema kuwa Jeshi la Polisi nchini Tanzania litaendelea kutoa msukumo
na kushirikiana na Interpol ili kusaidia katika mapambano ya uhalifu wa
kimataifa.
Kamishna Handani
ameutaja uhalifu ambao ni kero na kikwazocha uchumi kuwa ni pamoja na
Ugaidi, Uharamia, Biashara haramu ya dawa za kulevya na uhalifu mwingine
unaovuka mipaka.
Kamishna Hamdani
ambaye amekabidhiwa nembo maalum ya Interol, pia alipata fursa ya
kutembelea vitengo mbalimbali vya Makao makuu ya Interpol na kupatiwa
muhtasari wa mafunzo yanayotolewa na Interol katika kuwajengea uwezo wa
kiutendaji Maafisa na Askari wa kada mbalimbali.
Post a Comment