WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefanikiwa kukusanya sh. bilioni 83.4 kufikia mwaka 2013/2014 ambazo zinatokana na shughuli mbalimbali zilizofanywa na Idara ya Uhamiaji.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh Pereira Ame Silima wakati
wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam akieleza
mafanikio ya Wizara.
Mh
Pereira alibainisha kuwa kwa kipindi cha mwaka 2006/2007 zilikusanywa
shilingi bilioni 14.2 ambapo kumekuwa na ongezeko la bilioni 69.2
kufikia mwaka 2013/2014 ambayo ni moja ya mafanikio ya Serikali ya awamu
ya nne.
Mh
Pereira alibainisha kuwa Ongezeko hilo ni matokeo ya juhudi
zilizofanywa na Serikali katika kuboresha mifumo ya makusanyo ya
maduhuli kwenye vyanzo mbalimbali vya Wizara.
Aliongeza kuwa jumla ya magari 192 yalitolewa kwa idara hiyo, 93 yakiwa ni msaada ya wafadhili.
Alitaja
vifaa vingine vilivyonunuliwa kwa ajili ya Idara hiyo ni pikipiki 206
na boti mbili (02) ambazo hutumika kufanya misako na doria katika maeneo
mbalimbali nchini ikiwa ni hatua za maksudi katika kupambamna na
uhalifu.
Kwa
upande wa jeshi la Polisi, Mh. Pereira alisema kuwa wamefanikiwa
kupunguza uhalifu kutoka makosa 53,268 mwaka 2005 hadi kufikia 45470
mwaka 2013.
Alitaja
sababu kubwa ya kupungua kwa vitendo vya uhalifu nchini kuwa ni
ushirikiano mzuri toka kwa wananchi kwa kutumia mfumo wa ulinzi
shirikishi,utii wa sheria bila shuruti,vifaa vya kisasa kwa askari
yakiwemo magari, pikipiki na boti kwa ajili ya doria.
Wizara
ya Mambo ya Ndani ya nchi inaundwa na Jeshi la Polisi,Jeshi la
Magereza,Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Idara ya Uhamiaji,Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa,Idara ya Huduma kwa Jamii.
Post a Comment