Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kiongozi maarufu wa kisiasa kurukwa na akili 2014

 
Alhaj Maalim Hassan
********
Mrithi wa aliyekuwa mtabiri na mtaalam wa nyota wa Afrika Mashariki, marehemu Sheikh Yahya Hussein, ametabiri kiongozi mmoja wa kisiasa na mwenye nguvu kubwa katika jamii, atarukwa na akili mwishoni mwa mwaka huu.

Hayo yalisemwa na Alhaj Maalim Hassan, alipokuwa akizungunza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

“Natabiri kuna kiongozi mmoja wa kisiasa mwenye nguvu katika jamii hapa nchini, atarukwa na akili kuelekea mwisho wa mwaka huu na itakuwa anguko lake na wafuasi wake kwenye harakati za kuimarisha ustawi wa Watanzania na dola yake,” alisema Alhaj Hassan.



Hata hivyo, Alhaj Hassan hakutaja jina la kiongozi huyo na sababu zitakazosababisha arukwe na akili.

Aidha, alitabiri kuwa mchakato wa Katiba mpya utapita kwa mbinde hususan suala la muundo wa serikali tatu katika Muungano.

Hata hivyo, alisema baada ya malumbano hayo, Rais Jakaya Kikwete, atatumika zaidi kuweka mambo sawa lakini ni baada ya jamii nzima kuweweseka.

Pia, alisema mwaka huu si mzuri kwa viongozi wa kidini kwani kuna watakaokufa ghafla na baadhi yao wakiondolewa madarakani kwa aibu na kashfa.
Kadhalika, utabiri unaonyesha kuwa mwaka huu hususan siku za Jumatano, kutakuwa na shida kubwa na nyingi ikiwamo kuibuka kwa maradhi.

Kwa msingi huo, Alhaj Hassan aliishauri serikali kuchukua tahadhari katika kukabiliana na maradhi hayo yakiwamo malaria, kuhara damu na kichocho.
“Kwa asilimia kubwa, utabiri uliopita wa mwaka 2013 ulikamilika kwa asilimia 90 na mengi niliyoyatabiri mwaka jana yametokea kwani kuna mashujaa waliofariki dunia, ajali nyingi za barabarani, angani na baharini watu kuwa na hofu na wengine kuuawa,” alisema Alhaj Hassan. 

CHANZO: NIPASHE
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top