Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Bwa. Suluhu Ali Rashid,
akitowa maelezo kwa mgombea wa CCM alipofika kuchukua fomu ya kugombea
Uwakilishi katika Ofisi za Tume Maisara.
Akionesha fomu zake baada ya kukabidhiwa na Afisi wa Tume ya Uchaguzi
MGOMBEA nafasi ya Uwakilishi katika Uchaguzi
mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Bwa,Mahmoud Thabit Kombo, akikabidhiwa Fomu ya kugombea nafasi hiyo na Msimamizi
wa Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki Suluhu Ali Rashid, makabidhiano hayo
yamefanyika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Maisara
Mgombea wa Uwakilishi katika uchaguzi mdogo wa jimbo la kiembesamaki Bwa
Mahmoud Thabit Kombo akionesha Fomu zake za kugombea nafasi hiyo ya
Uwakilishi ya Jimbo la Kiembesamaki baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa
Uchaguzi
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Kiembesamaki Bwa. Mahmoud Thibit Kombo akishindikizwa na Wanachama wa
CCM wa jimbo la Kiembesamaki baada ya kuchukuwa Fomu za kugombea
Uwakilishi kupitia uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mwazoni mwa
mwezi wa Febeary 2014, kuziba nafasi ilioachwa wazi na Mhe. Mansoor
Yussuf Himid aliyevuliwa Uwanachama wa CCM na Chama chake mwaka jana.
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Bwa Nahamoud Thabit Kombo akiondoka
katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi kwa kushindikizwa na wapanda Pikipiki
kuelekea katika Ofisi za CCM tawi la Kiembesamaki kwa mazungumzo na
Wanachama wa CCM wa Jimbo la Kiembesamaki.Picha Zote na Othman Mapara-Zanzibar
Post a Comment