RPC Mungi
..................................................
NA
DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
JESHI
la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu wawili kwa makosa mawili tofauti
likiwemo la Wilson Mbilinyi (25) mkazi wa Barabara mbili kata ya Makorongoni
wilaya ya Iringa kukutwa na madawa ya kulevya.
Akizungumza
na mtandao wa www.matukiodaima.com
ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo lililotokea januari 16 majira ya saa 5 kamili asubuhi.
Mungi
alisema mtuhumiwa huyo alikutwa na kete 15 zinazozaniwa kuwa ni madawa ya
kulevya aina ya kokeini.
Wakati
huohuo jeshi la polisi mkoani Iringa lilimkamata raia wa Ethiopia Dasala Halute
(20) kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Kamanda
Mungi alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 16 januari mwaka huu majira ya
saa 3:30 usiku maeneo ya Ipogolo kata ya Ruaha.
Credit: www.matukiodaima.com
Post a Comment