Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto)
akimsikiliza Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba (wa pili
kushoto) wakati alipokuwa akimtambulisha dada zake,wakati Mh Lowassa
alipokwenda kumpa pole Mzee Makamba aliepatwa na msiba wa kufiwa na mama
yake mzazi huko kijijini kwake Maezangula wilaya ya Korogwe,Mkoani
Tanga jana.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
(katikati) na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia,Mh. January Makamba
wakati wa mazungumzo yao.Mh Lowassa aliitembelea Familia ya Mzee Makamba
kwa kumpa pole kwa kupatwa na msiba wa kufiwa na mama yake mzazi huko
kijijini kwake Maezangula wilaya ya Korogwe,Mkoani Tanga jana.
Post a Comment