Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwenye kikao na
watumishi wa idara ya afya wa hospitali kuu ya Mkoa iliyopo katika
Manispaa ya Sumbawanga. Alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kusikiliza
kero, malalamiko pamoja na ushauri kwa ajili ya kuboresha huduma na
utendaji katika hospitali hiyo. Kero mbalimbali zilitolewa ikiwepo
upandishwaji wa vyeo kuchukua mda mrefu, kubadilishiwa muundo wa vyeo na
kusababisha kupungua kwa mishara kimakosa, uhaba wa vitendea kazi
pamoja na madaktari bingwa wa upasuaji ambapo kwa sasa hamna hata mmoja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya baada
ya kusikiliza kero mbalimbali aliagiza uongozi wa hospitali hiyo
kutatua kero zilizo chini ya uwezo wao na zile nyingine kuahidi
kuzitafutia ufumbuzi kwa kuzishirikisha mamlaka husika. Kushoto ni
Mganga Mkuu hospitali ya Mkoa Rukwa Dkt. William Gurisha. Kero nyingi
zimeonekana kuibuka kutokana na uhaba wa fedha za OC kutofika kwa wakati
na kwa kiwango kilichopangwa. Hata hivyo hospitali hiyo imeonekana
kujipanga kutumia vyanzo vya mapato ya ndani kutatua baadhi ya kero
hizo.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla akifafanua baadhi ya mambo ya kiutawala katika kikao hicho.
Wajumbe katika kikao hicho.
Mmoja ya wahudumu wa afya akitoa kero yake.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
Post a Comment