Mwaka 2013 ulianza kwa kushtua katika sekta ya elimu baada ya matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 kutolewa Februari mwaka huu.
Matokeo hayo yaliibua mjadala mpana sana kuhusu
mustakbali wa elimu nchini, ambapo asilimia 66 ya watahiniwa walipata
daraja sifuri.
Mjadala huu ulitoa nafasi kwa Serikali na wananchi kukaa chini na kubaini nini cha kufanya ili kuinusuru sekta ya elimu.
Matokeo hayo yalikuwa ni mabaya ukilinganisha na
mwaka mwaka 2009 ambapo jumla ya wanafunzi 195,000 sawa na asilimia 78
ya wahitimu wote walipata daraja sifuri na daraja la nne.
Pia mwaka 2010 wanafunzi 310,000 ambao ni zaidi ya asilimia 60 ya wahitimu wote walipata madaraja hayo ya chini kabisa.
Uchunguzi wa matokeo
Baada ya matokeo ya mwaka huu, Serikali iliamua
kuunda kikosi kazi cha kuchunguza chanzo cha matokeo hayo mabaya.
Watanzania wengi walidhani hatua hiyo ingekuwa moja ya njia ya kuwapatia
vyanzo vya kina kuhusu kufeli kwa wanafunzi.
Hata hivyo, badala yake Serikali ikatumia
mapendekezo ya ripoti ya awali ya tume ya uchunguzi kufuta matokeo ya
kidato cha nne yaliyokwishatangazwa.
Aidha, ililiamuru Baraza la Mitihani Tanzania
(Necta) kuyachakata upya kwa kutumia mfumo wa zamani, kwa kisingizio
kuwa mfumo mpya uliokuwa umetumika kutokuwa na maandalizi na wala
haukuwa umefanyiwa utafiti wa kutosha kabla ya kutumika.
‘Daraja la tano’
Baada ya matokeo mabovu ya kidato cha nne mwaka 2012, Serikali ilikuja na mkakati mwingine wa kubadilisha madaraja ya ufaulu.
Akitangaza mabadiliko hayo, Katibu Mkuu wa Wizara
ya Elimu, Profesa Sifuni Mchome alisema hatua hiyo ilitokana na maoni
yaliyokusanywa kutoka kwa wadau wa elimu. Pamoja na mambo mengine,
alisema Serikali imefuta daraja sifuri na badala yake kutakuwepo na
daraja la tano.
MWANANCHI
Post a Comment