Hali ya
wanawake inazidi kuwa mbaya ndani ya nchi yao TANZANIA inayosifiwa kuwa
ni Kisiwa cha Amani (Amani kwa wanaume) Tukio hili lilitokea mapema
mwezi wa nane mwaka huu Kijiji cha Nyantira Tarime Mara. Katika
mazungumzo yake huyu binti alisema kwamba anatamani sana kurudi nyumbani
kwa wazazi wake, tatizo ni kwamba kwa kuwa alilipiwa MAHARI na mume
wake (aliyemkata panga mguu na kuutoa) hawezi kurudi kwao , wala mama
yake hawezi kumkubalia arudi kwao ni mpaka baba yake aje atoe ruhusa ya
yeye kurudi nyumbani au abaki kwa mume muuaji avumilie-MFUMO DUME
UMEKAMATA MIZIZI (mbayaaaaa, sanaaaa. anajisemeaga Mch Rwakatare)<>
Samahani
kwa picha mbaya, lakini hatuna budi kuonyesha unyama uliopita kipimo
ambao wanawake wanaupitia. Na huu ni mfano halisi kwa mwanamke huyu wa
Tarime Musoma. picha ya juu ni kipande cha mguu wa huyo binti ambao mume
alipitisha panga mithili anakata muwa, picha inaonyesha mguu uliobaki
na mguu wa kushoto pia ulikatwa lakini haukutoka, pamoja na mkono wake
wa kushoto ulikatwa lakini haukutoka. ( Kumbuka tupo kwenye maandalizi
mazito ya kuandimisha siku 16 za kupinga ukatili dhili ya Wanawake)
Mama
mzazi wa binti aliyekatwa mguu na mkwe wake akilia kwa uchungu mkubwa
alipokuwa anaelezea kisa kilichomkumba binti yake. Ni huzuni kubwa sana
ukivaa viatu vya familia hii. Mama anasema kwa utamaduni wao baba wa
mtoto aliyekatwa yaani mume wake ndiye mwenye dhamana ya kuamua mtoto
arudi nyumbani au aendelee kubaki ka mume fedhuli aliyemgeuza mwenzake
ni pingili la muwa au kitoweo Bucher.
Juu ni
mama na chini ni binti akiwa na mawazo juu ya kupoteza mguu wake kwa
sababu tu mume kaamua kuukata. Huyu binti ameathirika sana kisaikolojia
kutokana na tatizo hilo la kukatwa mguu wake na mume wake. hivyo anaomba
asaidiwe arudi nyumbani kwa wazazi wake, au popote pa kuishi ilimradi
aondolewe kwenye mazingira yale aliyopatia mkasa huo. Mbaya zaidi baba
mkwe wake anamwambia "wewe unaona raha kulala kitandani wakati mtoto
wangu analala chini jela) kwa kauli hiyo huyu binti yupo hatarini zaidi.
wanaweza kumuua wapoteze ushaidi. hata hivyo binti aligusia sababu ya
kufanyiwa unyama huo ni mwanaume kuwa na mwanamke mwingine na kwamba
alishahamishia mapenzi huko, na kumuona yeye kama dudu mtu. (Wakati
tunaendelea na maadhalizi ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya
Wanawake, bado hali ni tete)
Hawa ndio
Washika dau wetu wakubwa serikalini. wanasimamia Wizara ya Jinsia
Maendeleo ya Jamii na Watoto. jamani waheshimiwa sana mko wapi? huku
wanawake twafaaa, mnatusaidia vipi? viti vya bunge vinakalika vipi kwa
hali hii? ni lini wanawake tutapaza sauti zetu ili dunia ijue unyama huu
unaoendelea dhidi ya wanawake wa Tanzania? Wanawake Hatuna AMANI kabisa
ndani ya nchi yetu. Wizara na Taasis mbalimbali, Wadau wa kutokomeza
ukatili dhidi ya Wanawake, kuna jinsi ya kumsaidia huyu mama kwa
kumuondoa pale kwenye ile nyumba alimofanyiwa UNYAMA huu na akapewa
makao salama? Usikose kufuatilia Joyce Kiria Wanawakelive EATV na hapa
kwenye ukurasa wetu, ili upate mkasa huu wakati tunajipanga kuendelea na
mapambano ya Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake.
-credit wanawake live tv
Post a Comment