Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakiwa katika picha ya Pamoja na
Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini Ikulu
jijini Dar es Salaam leo jioni(picha na Freddy Maro)
………………………………………………………………………………………
By Freddy Maro
Washirika wa
Maendeleo wa Tanzania wakiwemo baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi
zao hapa na mashirika ya Kimataifa wameelezea kuridhishwa kwao na juhudi
za Serikali ya awamu ya Nne ya Tanzania inaoongozwa na Rais Dkt.Jakaya
Kikwete, katika mapambano dhidi ya Rushwa nchini.
Hayo yameelezwa
na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue mara baada ya kukutana na
baadhi ya Mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa ikiwemo
Banki ya Afrika,Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la
Kimataifa(International Monetary Fund) ikulu jijini Dar es Salaam leo
jioni.
“Yaliyojitokeza
katika mkutano huu ni wao kutambua juhudi za serikali yetu kuimarisha
vita dhidi ya rushwa ka kuimarisha taasisi zinazohusika moja kwa moja
kwa kuziongezea bajeti na kuajiri wafanyakazi wenye uwezo na ujuzi wa
kutenda kazi kwa weledi.Ofisi hizi ni pamoja na TAKUKURU yenyewe, ofisi
ya mwendesha mashtaka, Mahakama, sekretarieti ya maadili ya umma na
polisi,” alisema Balozi Sefue.
Katibu Mkuu
Kiongozi amesema kuwa washirika hao wa maendeleo wamefurahi kutambua
kwamba Serikali imeongeza idadi ya watumishi wa umma wanaofanya kazi
katika taasisi zinazohusika na vita vya rushwa nchini na kuboresha
utendaji baada ya kupata mafunzo na kwamba miundo mbinu ya taasisi hizi
ikwemo majengo ya ofisi na vitendea kazi vimeimarishwa.
Balozi Sefue
aliongeza kusema kuwa washirika hao wa maendeleo wamekuwa wawezeshaji
wakuu wa taasisi zinazopambana na rushwa nchini kwa kuzichangia kwa
fedha na kugharamia mafunzo ya baadhi ya watumishi wa taasisi hizo na
kwamba katika mkutano wa leo wameahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za
Tanzania katika vita dhidi ya Rushwa kwa kuisaidia serikali kuimarisha
mifumo, sheria, taratibu na kutoka mafunzo kwa watumishi.
Baadhi ya
Washirika wa Maendeleo waliohudhuria mkutano wa Katibu Mkuu kiongozi ni
pamoja na wawakilishi kutoka Jumuiya ya Ulaya EU, Balozi wa Unigereza
nchini, Balozi wa Canada,Balozi wa Norway,Balozi wa Finland, Balozi wa
Denmark,Balozi wa Ujerumani, Balozi wa Ireland, Balozi wa Sweden,
Mwakilishi wa Ubalozi wa Japan, Mwakilishi wa Benki wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika, mwakilishi wa Benki ya Dunia na Mwakilishi wa
Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).
Post a Comment