WATU 37 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA KOSA LA KUNYWA POMBE KABLA YA MUDA.
JESHI
LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 37 KWA KOSA LA KUNYWA POMBE
KABLA YA MUDA. WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MATUKIO MATATU TOFAUTI
KATIKA JIJI NA MKOA WA MBEYA MNAMO TAREHE 22.01.2014. KATIKA TUKIO LA
KWANZA SOPHIA BOLINGO (27) MKAZI WA SINDE ALIKAMATWA NA ASKARI POLISI
AKIWA NA WENZAKE 06 KATIKA KILABU CHA POMBE KIITWACHO NGOMA NZITO, KATA
YA SINDE, TARAFA YA SISIMBA WAKIWA WANAKUNYWA POMBE MAENEO HAYO KABLA YA
MUDA. KATIKA TUKIO LA PILI DENIS BUJA (19) MKAZI WA KABWE JIJINI MBEYA
ALIKAMATWA NA ASKARI POLISI AKIWA NA WENZAKE 07 WAKIWA WANAKUNYWA POMBE
KATIKA KILABU KIITWACHO MNYONGE MAENEO HAYO. KADHALIKA KATIKA TUKIO LA
TATU FRANK ASUKILE (24) MKAZI WA SIMAMBWE KATA NA TARAFA YA TEMBELA,
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI PIA ALIKAMATWA AKIWA NA WENZAKE 21 WAKIWA
WANAKUNYWA POMBE MAENEO HAYO KABLA YA MUDA. WATUHUMIWA WOTE WAMEFIKISHWA
MAHAKAMANI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUNYWA POMBE KATIKA MAENEO
TOFAUTI KABLA YA MUDA ULIOWEKWA KISHERIA KWANI KUFANYA HIVYO NI KINYUME
CHA SHERIA NA JESHI LA POLISI KAMWE HALITAFUMBIA MACHO VITENDO KAMA
HIVYO VILIENDELEE KUTOKEA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTUMIA MUDA HUO
KUFANYA SHUGHULIA MBALIMBALI ZA KIMAENDELEO.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment