KATIKA
kile kinachoonekana kama kumsafisha Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe dhidi ya kashfa ya
uzinzi inayomuandama.
Mwanasheria
Mkuu wa chama hicho, Tindu Lissu amesema suala hilo ni maisha binafsi
ya mtu, ambayo hayawezi kuhusishwa na wadhifa wake kwa namna yoyote.
Akizungumza
katika mahojiano maalum ndani ya chumba cha habari cha Global
Publishers Ltd, Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam juzi, Lissu alisema
kwa kadiri anavyofahamu, suala hilo ni binafsi linalopaswa kuachwa
chumbani, kwa sababu kama litahusishwa na nafasi yake, ni sawa na
kukubali kuwa mzee Nelson Mandela wa Afrika Kusini si lolote wala
chochote.
“Maisha
ya kimapenzi ya mzee Mandela yalikuwa ya ukakasi, kwa maana hiyo
unataka tuseme kuwa kwa sababu hiyo, mzee huyu hakuwa kiongozi bora,
unataka tuseme Bill Clinton wa Marekani hakuwa kiongozi bora kwa sababu
tu alipata kashfa katika moja ya makorido ya Ikulu ya White House? Mimi
nadhani haya mambo kama yapo au hayapo, hayahusiani na uwezo wa mtu
kiuongozi, ni mambo ya chumbani yanayopaswa kuachwa huko,” alisema
Lissu.
Lissu
alikuwa akirejea baadhi ya sababu zilizosababisha mgogoro kati ya chama
chake na Naibu Katibu Mkuu wao aliyetimuliwa, Zitto Kabwe, anayedaiwa
kushiriki kuandaa waraka wenye nia ovu, ambao pamoja na mambo mengine,
ulitaka kufanyika kwa mabadiliko ya viongozi wa juu, akiwemo Mwenyekiti
wa Taifa, kwa kudaiwa kuwa na elimu ndogo pamoja na kukosa uaminifu
katika ndoa yake.
Aidha,
hivi karibuni wakati wa kikao kilichomalizika cha Bunge mjini Dodoma,
Freeman Mbowe alidaiwa kuvuruga ziara ya mbunge mmoja mwanamke (wa viti
maalum) wa chama chake aliyekuwa katika ziara ya kibunge nje ya nchi, na
badala yake kumtaka kuungana sehemu alipokuwepo.
Mbunge
huyo wa Singida Mashariki, licha ya kukiri kuwepo kwa mgogoro
unaokitikisa chama chao, lakini alisema hatimaye Chadema itashinda na
kubakia imara na akasisitiza kuwa mwavuli wa mahakama alionao Zito
ukiondoka, watamtimua.
Chanzo: http://www.globalpublishers.
Post a Comment