Naibu Waziri wa Madini Mh. Steven Masele akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wekezaji waliofika ofisini kwake.
………………………………………………………………………………………..
Kutokana na ugunduzi wa gesi asilia na mafuta nchini, Tanzania imeonekana kuwa na thamani kwa nchi mbalimbali duniani na kuiangalia nchi hii kwa namna tofauti na ilivyokuwa awali kwani sasa imeonekana kuwa na utajiri mkubwa.
Ugunduzi
huu umepelekea Wizara ya Nishati na Madini kupokea wageni
wanaowakilisha nchi na watu binafsi wanaofika ili kutafuta fursa za
kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano ya kibiashara baina
ya nchi husika.
Hivi karibuni wizara ya Nishati
na Madini imetembelewa na ujumbe toka Jamuri ya Czech nchi ndogo
miongoni mwa nchi zinazounga umoja wa ulaya waliofika kwa lengo la
kutafuta fursa za kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kudumisha uhusiano
baina ya nchi hizi mbili.
Ujumbe huu uliongonzwa na Bw.
Tomas Dub Naibu Waziri wa mambo ya Nje ya Nchi ya Czech aliyeelezea
uwezo wa nchi yake katika masuala ya nishati na madini na kusema kwamba
awali nchi yao ilijikita katika umeme uliozalishwa kwa maji, gesi pamoja na nishati jadidifu, na kusema kwamba wana wataalamu wa kutosha katika sekta ya nishati.
Dub
alieleza kuwa maendeleo si tu kutegemea utafutaji na uzalishaji wa gesi
asilia bali inatakiwa nchi ifanye nguvu ya ziada katika kuongeza
thamani ya bidhaa hiyo na hilo litawezekana tu kwa kujenga viwanda jambo
lililowavuta ili kuja kutafuta fursa hiyo nchini.
Dub alikamilisha mahojiano hayo kwa kuitaka Wizara kuelimisha
watanzania katika chuo cha madini katika nchi hiyo na kwamba
mawasiliano yataendelea kufanyika ili kufikia malengo ya uhusiano huo.
Kwa upande wake Masele amesema kwamba zipo fursa nyingi za uwekezaji nchini katika sekta ya madini na
zaidi madini ya viwandani lakini pia sekta ya nishati kwa kufuatia
ugunduzi wa gesi na mafuta vitalu vimetangazwa hivyo ni fursa kwa Czech
kuomba vitalu hivyo ili kuweza kushiriki katika shughuli za utafutaji wa
mafuta na gesi.
Post a Comment