Afisa
Mfawidhi SUMATRA Kanda ya Ziwa Japhet Leisimaye Ole akiwatuliza abiria
ambao walikuwa wakihitaji kusafiri katika eneo la Kamanga kufuatia mgomo
wa wafanyakazi wa kivuko cha MV. Orion.
'Abiria wetu tunawaomba mtuvumilie, tunahitaji haki zetu' Lilisomeka moja ya bango la waaandamanaji hao.
Safari ilisitishwa kwa muda mpaka kieleweke.
Mv. Orion
Kapteni
wa MV. ORION Adam Yusuph akiongoza meli yake huku Afisa Mfawidhi wa
SUMATRA Kanda ya Ziwa Japhet Leisimaye Ole akijiridhisha juu ya
ubora wa usafiri huo katika utoaji huduma.
Safari inasonga.
Ratiba.
Mfanyakazi wa Kamanga Ferry akitoa maelekezo kwa abiria jinsi ya kuvaa jaketi la kujiokoa wakati wa ajali.
Safari imefikia ukingoni.
Mahojiano na wananchi.
Hatimaye mgomo umepatiwa
utatuzi nacho chombo kinaendelea na utoaji huduma.
Mwandishi,William Bundala wa matukiodaima.com ,Mwanza
......................................................................................................
WATUMISHI wa
Kampuni ya Kamanga Fery ya Wilayani Sengerema leo wameweka mgomo
ukishinikiza kuondolewea kwa watumishi wenzao wawaili na kusimamisha
utowaji huduma ya usafiri wa abiria na magari Jijini hapa.
Hatua
hiyo ilielezwa na Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi Adamu Yusufu
ambaye pia ni Kepteni wa kivuko cha MV Orion cha Kampuni ya Kamanga Fery
Ltd. kinachotoa huduma kati ya Kamanga Wilayani Sengerema na Kamanga
Jijini Mwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye ofisi za kampuni hiyo Mwenyekiti Kapteni
Yusufu alisema kwamba wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa ujumla wao
wameamua kugoma kutoa huduma ili kushinikiza Mkurugenzi Wiebke Gaetye
kuwaondoa watumishi Renatus Manyanda (Meneja rasilimali watu) na Anna
Malapa (Mhasibu matumizi) kutokana na kuwanyanyasa wafanyakazi wa
Kampuni hiyo.
Mwenyekiti
huyo alitaja sababu za mgomo huo kuwa ni pamoja na Manyanda kuwafukuza
watumishi bila kosa, kushindwa kulipa makato ya mishahara yao kwenye
Mfuko wa Jamii (NSSF), kushindwa kulipa mishahara zao kwa wakati ambapo
wanadai tangu mwezi Novemba mwaka jana na kushindwa kufanya matengenezo
ya vivuko vya kampuni hiyo kwa wakati.
“Bila
Mkurugenzi kuyashughulikia haya tunayolalamikia ikiwa ni pamoja
na kutuondolea watumishi hawa wanaolalamikiwa na wenzao, nasi hatuko
tayari kufanya kazi na tutaendelea na mgomo hadi kilio chetu
kitakaposikilizwa na kutolewa majibu” alisisitiza.
Kwa
upande wa Mhasibu Malapa alisema kwamba amekuwa akiwanyima malipo
yanayoizinishwa na Mkurugenzi ama uongozi wa Kampuni hiyo na hata
amekuwa akitoa kauli za kuwakejeli watumishi wenzake jambo ambalo
wamedai kuchoshwa nalo.
Kufatia
mgomo huo uliodumu kwa masaa kadhaa na kupelekea Mkurugenzi Gaetye
kuchukua jukumu la kukaa na wafanyakazi ili kusikiliza hoja na
malalamiko yao ambapo aliamua kumfukuza kazi kwanza Manyanda kisha
kusikiliza malalamiko mengine ili kupoza hasira za wafanyakazi hao.
Akizungumza
madai ya wafanyakazi hao Mkurugenzi huyo alisema kwamba tayari
amemfukuza kazi huku hoja za malipo ya mishahara yao ataifanyia kazi
haraka na ile ya NSSF huku Mhasibu Malapa akisimamishwa kwanza
kuchunguzwa na uamuzi wake ukisubili kikao cha uongozi wa Kampuni.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi (Cotwu) tawi la Kampuni hiyo
Kapteni
Jorwa Magesa (MV Orion) alisema kwamba kufatia kikao na Mkurugenzi wao
wamelidhika na hatua alizochukua na wamempatia muda kushughulikia mambo
mengine yaliyosalia ikiwa ni malalamiko yao ya msingi.
Hatua
ya kuondolewa kwa Manyanda imepongezwa na wafanyakazi na wananchi wa
Kijiji cha Kamanga Wilayani Sengerema ambao juzi majira ya jioni
waliandamana na mabango kumpinga kuendelea kuwa mfanyakazi wa Kampuni
hiyo hali hiyo ilipelekea jana
kuwepo mgomo mkali kwa wafanyakazi hao nao wakipinga kuendelea kuwepo
kwa watu hao katika Kampuni hiyo.
Manyanda
pia amelalamikiwa na baadhi ya wafanyakazi waliokataa kutajwa majina
yao hadharani kwa madai kuwa Manyanda alikuwa akitumia pia Jina la Mama
Salma Kikwete kumtishia Mkurugenzi huyo raia wa Taifa moja la Ulaya kuwa
akimfukuza naye ataondolewa nchini.
Hadi
tunakwenda mitamboni hali ya eneo la Kamanga fery ilikuwa shwari baada
ya Mkurugenzi na wafanyakazi wake kukubaliana kuendelee kutolewa huduma
ya usafiri wa abiria na magari wakati madai yao mengine yakishughulikiwa
na kuchukuliwa hatua za haraka kama walivyokubaliana.
Post a Comment