RPC Mungi
............................................................................
NA DIANA
BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
Watu
watatu wamefariki dunia katikamatukio matatu tofauti likiwemo la motto Iddy
Mwimbage (5) mkazi wa Idodi kata ya Mlowa wilaya ya Iringa vijijini kutumbukia
ndani ya kisima.
Akizungumza
na mtandao wa www.matukiodaima.com
ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo.
Kamanda
Mungi alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 16 januari mwaka huu
majira ya saa 4 kamili asubuhi ambapo motto huyo alikuwa anacheza na wenzake
pembezoni mwa kisima hicho.
Wakati
huohuo mwanafunzi wa chuo cha ufundi cha Donbosco Vivian Kanuwa (19) mkazi wa
Kihesa kata ya Kihesa mkoani Iringa alikutwa amejinyonga chumbani kwake kwa
kutumia kamba ya katani.
Kamanda
Mungi alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 16 januari mwaka huu majira ya
saa 1:15 usiku ambapo marehemu alijinyonga baada ya kuchoshwa na manyanyaso ya
mama yake.
Aidha
Kamanda Mungi alisema mbali na matukio hayo mawili, mtoto Debora Tagalile(9)
ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Tagalile kata ya Ugwachanya wilaya ya
Iringa vijijini alifariki dunia baada ya kugongwa na gari majira ya saa 10
kamili jioni.
Kamanda
Mungi alilitaja gari hilo aina ya mitsubish canter lenye namba za usajili T 707
AJU, mali ya Masud Kilagwa mkazi wa Iringa lililokuwa likiendeshwa na Herbert
Vitus (44) mkazi wa kijiji cha Ikonongo, chanzo kikiwa ni mwendo kasi.
Post a Comment