Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi.
……………………………………………………………………………………
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe ameahidi kuboresha
maslahi ya Askari Polisi jambo ambalo litawezesha Jeshi la Polisi
kufanya kazi zake kwa ufanisi na hivyo kufanikiwa katika kukabiliana na
vitendo vya uhalifu.
Waziri
Chikawe aliyasema hayo jana Makao Makuu ya Polisi wakati alipokuwa
akizungumza na maafisa wakuu wa Jeshi hilo kwa lengo la kujitambulisha
baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa waziri wa wizara hiyo. Kikao hicho
kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi
Mhe. Pereila Amme Sillima, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbaraka
Abdulwakil, na viongozi mbalimbali wa wizara hiyo.
Aliongeza
kuwa, ataishawishi serikali iongeze bajeti ya Jeshi la Polisi ili
kuweza kuwajengea askari mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kuboresha
maslahi yao. Hii itasaidia kuongeza ufanisi, uaminifu na uadilifu katika
utendaji wao wa kila siku jambo ambalo litaleta maendeleo kwa wananchi.
Aidha
amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutanzua,
kubaini na kuzuia vitendo vya uhalifu katika Jamii kabla havijatokea ili
kuendelea kudumisha ulinzi na usalama hapa nchini.
Alisema
Jeshi la Polisi linahitaji sana ushirikiano kutoka kwa wananchi ambao
kwa kiasi kikubwa ndio wanaishi katika jamii ambayo inatendewa uhalifu
hivyo kupitia dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi ni vyema
wakaendelea kushirikiana na Jeshi hilo.
Vilevile
amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kutoa elimu juu ya sheria za
usalama barabarani kwa madereva hususan wa bodaboda ikiwa ni pamoja na
kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaokiuka sheria, kanuni na
taratibu hizo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu, amempongeza
Waziri Chikawe kwa kuteuliwa kwake kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, na kueleza kuwa ana imani kuwa waziri huyo atasaidia katika kuleta
mabadiliko ya kiutendaji hasa katika kuongoza mapambano dhidi ya
vitendo vya uhalifu pamoja na wahalifu.
IGP
Mangu alisema tabia za wananchi kujichulia sheria mkononi ni uvunjifu wa
sheria, hivyo wataendelea kuwachukulia hatua za kisheria kwa kuwakamata
wote wanaojihusisha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi ili
wafikishwe mahakamani.
Katika
kikao hicho IGP Mangu, alimkabidhi Waziri Chikawe hati ya mpango wa
maboresho unaoelekeza namna ambavyo jeshi la polisi linaendelea
kuboreshwa ili kuendana na usasa, weledi na lenye kushirikisha jamii,
pamoja na kitabu cha muongozo wa utendaji kazi wa jeshi hilo.
Post a Comment