Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI DKT HUSSEIN MWINYI AANZA RASMI KAZI

 



DSC_0559
Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akipokelewa Wizarani na Katibu Mkuu Bw. Job Masima.
 DSC_0563
Mhe. Mwinyi akisalimiana na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Samuel Ndomba mara baada ya kuwasili rasmi Wizarani. Kulia kwa Mnadhimu Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu Bibi Mwitango Rose Shelukindo. DSC_0573
Waziri Mwinyi akisalimiana na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo Wizarani.
DSC_0767
Mhe. Nahodha akisaini Hati ya kukabidhi Wizara ya Ulinzi na JKT kwa Waziri Mwinyi. Kutoka kulia waliosimama wakishuhudia ni Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Ndomba, Katibu Mkuu Bw. Masima na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Muhuga. DSC_0769
Mhe. Nahodha akikabidhi rasmi shughuli za Waziri wa Ulinzi na JKT kwa Mhe. Mwinyi. DSC_0772
Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi (wa tatu kutoka kulia) akiwa na watendaji wakuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT na Taasisi zake mara baada ya kukabidhiwa shughuli za Wizara hiyo.
…………………………………………………………………….
Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Bw. Job Masima leo amewaongoza wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi za wizara hiyo kumpokea Waziri wa Ulinzi Dkt Hussein Mwinyi (Mb) ambaye ameripoti wizarani hapo rasmi baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kushika wadhifa huo hivi karibuni.
Akimkabidhi wizara hiyo, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Shamshi Vuai Nahodha amemuasa Waziri Mwinyi kuwa pamoja na majukumu yake ni vema akatenga muda wa kutembelea miradi ya wizara hiyo, ikiwemo ujenzi wa nyumba ili kuona mambo yanavyokwenda na kurekebisha dosari kabla miradi haijafika mbali.
Kwa upande wake, Waziri Mwinyi amewataka viongozi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa kasi kubwa kwani kipindi kilichobaki ni kifupi sana kuelekea kwenye Uchaguzi mkuu ujao.
 “Mwaka uliobaki wa kufanya kazi ni mmoja tu kwani mwaka 2015 utakuwa na mambo mengi yanayohusiana na uchaguzi hivyo tulenge kufanya kazi kubwa kufikia malengo yetu ndani ya mwaka huu mmoja kwa kasi kubwa”, alisisitiza Mhe. Mwinyi.
Aidha, Mhe. Mwinyi alimshukuru Mhe. Nahodha kwa mambo muhimu aliyoshauri ikiwepo kukamilisha yale yote aliyokuwa ameyaanzisha kwa maslahi ya Wizara na Taasisi zake. Alimtakia  kila la heri katika majukumu yake ya uwakilishi na ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla ya makabidhiano hayo Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi walijipanga kwa safu ndefu kumpokea Waziri wa Ulinzi na JKT wakiongozwa na viongozi mbali mbali waliohudhuria makabidhiano hayo wakiwemo  Naibu Katibu Mkuu Bibi Mwitango Rose Shelukindo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Samuel Ndomba (aliyemuwakilisha Mkuu wa Majeshi), Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael Muhuga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mzinga Meja Jenerali Charles Muzanila na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Ulinzi na JKT.
Hii ni mara ya tatu kwa Mhe. Mwinyi kuteuliwa kuongoza Wizara hiyo. Kwa mara ya kwanza aliteuliwa mwaka 2008 hadi bunge lilipovunjwa wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Aidha, aliteuwa tena katika Baraza jipya mwaka 2010 hadi 2012 alipohamishiwa Wizara ya Afya.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ulinzi na JKT
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top