UONGOZI wa
Ashanti United ya Ilala umesema timu yao haiwezi kushuka daraja kwani ina
benchi la ufundi makini na wachezaji wenye uwezo.
Akizungumza jijini, Afisa Habari wa timu hiyo, Marijani Rajabu, alisema unawashangaa
watu ambao walianza kuiweka timu yao miongoni mwa timu zitakazo zushuka daraja
wakati ligi bado haijaanza mzunguko wa pili.
“Mzunguko wa
kwanza kweli timu haikufanya vizuri ndio maana uongozi uliliona na kufanya
mabadiliko kwenye benchi la uhaijaanza mzunguko wa pili.
“Mzunguko wa
kwanza kweli timu haikufanya vizuri ndio maana uongozi uliliona na kufanya
mabadiliko kwenye benchi la ufundi na kufanya usajili makini na sasa timu
imeshavuka mstari wa kushuka daraja”, alisema Marijani
Pia
aliwataka mashabiki kuwa wavumilivu pale timu inapofungwa kwani kufungwa mchezo
miwili siyo kigezo kuwa timu ni mbovu na kuanza kusema itashuka daraja.
Marijani
amesema wamejiandaa vema kuikabili Kagera Sugar kwenye mchezo ujao ambao
utachezwa Uwanja wa Chamazi, uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na
kuwaomba mashabiki kufika kwa wingi kuishangilia timu yao.
Post a Comment