Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea sehemu inayoingia maji ya chumvi katika eneo la Kilimani mjini Zanzibar, kushoto Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Mahmoud Mohammed Mussa.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma, akitoa maelezo mbele
ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
kuhusiana na kuingia maji ya chumvi katika eneo la Kilimani mjini Zanzibar.
Afisa
Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja Dr. Makame Ali Ussi, akitoa maelezo
mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif
Hamad, kuhusiana na kuingia maji ya chumvi katika eneo la Fungu refu,
Mkokotoni. Wilaya ya Kaskazini Unguja
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
akishuhudia hali ya uharibifu katika hoteli ya Zalu Nungwi, uliotokana
na upepo mkali uliovuma katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Jumapili usiku,
na kusababisha majengo na maeneo kadhaa kuharibiwa vibaya.
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea
skuli ya Nungwi, kuangalia uharibifu uliotokana na upepo mkali uliovuma
katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Jumapili usiku, na kusababisha majengo
na maeneo kadhaa kuharibiwa vibaya. (picha na Salmin Said, OMKR)
Post a Comment