Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MBEYA CITY YASHINDWA KUTAMBA UWANJA WA NYUMBANI YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA SIMBA, YANGA YAIBAMIZA KOMOROZINE 5-2

 




Timu ya Mbeya City, leo imeshindwa kutamba kwenye uwanja wa nyumbani wa Sokoine kwa kulazimishwa sare kwa kufungana bao 1-1 na Simba, mchezo uliokuwa na kila aina ya upinzani uliomalizika hivi punde Jijini Mbeya.  
Bao la Simba lilifungwa na Amis Tambwe katika kipindi cha pili huku bao la Mbeya City, likipatikana kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penati.


Huko kwingineko:- Ashanti United 0- 0 Kagera Sugar,  Ruvu Shooting 1 - 0 Coastal Union



HUKO Komorozine:- Timu ya Yanga leo tena imeweza kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliochezwa nchini Komorozine. Mabao ya Yanga yamewekwa kimiani na Mrisho Ngasaa, aliyeweza kuibuka tena kwa mara nyingine na 'Hut Trick' katika dakika ya 22, 87 na 90. Mabao mengine yalifungwa na Simon Msuva katika dakika ya 37 na Hamis Kiiza katika dakika ya 13.


HABARI KAMILI:
Mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa baina ya vilabu vya Simba na Mbeya City uliochezwa jioni ya leo katika dimba la Sokoine umemalizika bila mbabe.

Katika mchezo huo Mbeya City ndio walioanza kuliona lango la Simba katika dakika ya 17 kwa mkwaju wa penati, bao hilo lilidumu mpaka mapumziko wenyeji wakitoka kifua mbele.

Kipindi cha pili Simba walianza kwa kasi na hatimaye katika dakika ya 50, mshambuliaji hatari wa Simba Mrundi Amiss Tambwe akaifungia timu yake bao la kusawazisha.

Timu hizo ziliendelea kushambuliana lakini mpaka mwamuzi wa mchezo huo anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalibaki moja kwa Mbeya City na moja kwa Simba.

KUTOKA COMORO
Mabingwa wa Tanzania bara na wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la mabingwa wa Afrika Dar Young African imefanikiwa kuvuka kwenda raundi ya pili ya michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Komorozine De Domoni mabao 5-2.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Mrisho Ngassa aliyefunga hat trick, huku Hamis Kiiza na Msuva wakifunga bao moja moja.
Yanga sasa watakutana na timu kubwa ya Misri Naciona Al Ahly. 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top