Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TASWIRA ZAIDI ZA KUAGWA KWA IGP MSTAAFU SAID MWEMA

 

 IGP Mstaafu Said Mwema akiwa katika Gari Maalum la wazi huku akipunga mikono kwa Maafisa, Askari, Wageni Waalikwa na Wananchi mbalimbali katika hafla fupi iliyofana sana ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma. Sherehe hizo zimefanyikia katika Viwanja vya Polisi Barracks Jijini Dar es Salaam.
 IGP Mstaafu Said Mwema(kushoto) akimkabidhi kitara IGP Mpya wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu(kulia) ikiwa ni ishara ya Makabidhiano ya Madaraka ya Uongozi wa Jeshi la Polisi hapa Nchini. Sherehe hizo zilizopambwa na Gwaride Maalum lililounndwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi imefana sana katika Viwanja vya Polisi Barracks Jijini Dar es Salaam.
 Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakipunga mikono wakati IGP Mstaafu, Said Mwema(hayupo pichani) akipita katika Gari Maalum la wazi. Hafla hiyo fupi imefanyika kwa ajili ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma(wa Nne toka kulia) ni Mkrugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid(tatu toka kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kulia) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile).
 IGP Mstaafu, Said Mwema akipokea Salaam ya heshima na utii iliyotolewa na Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi(hawapo pichani) katika hafla fupi ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Jeshi la Polisi kwa kumjibu wa Sheria. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 15, 2014 katika Viwanja vya Polisi barracks Jijini Dar es Salaam.
 IGP Mstaafu, Said Mwema akikagua Gwaride Maalum alililoandaliwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi katika hafla ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Jeshi la Polisi kwa kumjibu wa Sheria.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top