Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TANGAZO MUHIMU KWA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

 


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE MAALUM
TAARIFA KWA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA _______________________________________________
 Kufuatia wito wa Serikali kuwa Wajumbe wote wanaombwa kufika Mjini Dodoma kuanzia tarehe 16 Februari, 2014 katika Viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar wanapenda kuwaarifu Wajumbe wote maandalizi yafuatayo: -
1.0        USAFIRI WA KUFIKA DODOMA 
Wajumbe wote wanatakiwa kujigharamia wenyewe kufika Dodoma kwa vyombo vya usafiri wa umma.  Wajumbe watarejeshewa gharama za usafiri wa kufika Dodoma kutoka maeneo wanayotoka baada ya kuwasilisha stakabadhi za gharama walizotumia kwa usafiri.
2.0        MALAZI
Utaratibu wa malazi umeandaliwa.  Hoteli zilizoteuliwa kwa malazi kwa Wajumbe kuchagua kwa kadri itakavyowapendeza zimeainishwa.  Hoteli hizo ni hizi zifuatazo: - 
NA.
JINA LA HOTELI NA MAHALI ILIPO
IDADI YA VYUMBA
MAWASILIANO
1.
Dodoma Hotel - Mjini
87
0262321641
0262353782
2.
St Gaspar Conference Centre - Kisasa
73
026235226
0767999903
3.
Hotel Fifty Six - Viwandani
53
0757202630
0713702066
4.
Four Points Hotel - Kisasa
20
026 2350214
0757  613270
5.
Peter Palm Hotel
22
0767888311
0784888311
6.
Cana Lodge - Mjini Barabara ya 9
17
026 2321199
0713 786611
7.
Dodoma Grand Hotel - Majengo
20
026 2321187
NA.
JINA LA HOTELI NA MAHALI ILIPO
IDADI YA VYUMBA
MAWASILIANO
8.
Kingstone Lodge
17
026 2323057
9.
Hotel DM - Majengo
19
0712 447325
10.
Golden Glory Guest House - Area C
11
026 2353343
11.
Modern Hotel - Area C
35
026 2304466
12.
Nam Hotel - Area C
28
0756  652659
026 2354467
13.
Marryland Hotel - Area C
20
0757 919166
19.
Giftland Hotel - Area C
48
0762 159099
20.
Golden Crown Hotel - Area C
27
0757 760333
21.
Joanic Hotel - Kisasa
33
0653  867026
22.
Kidia Vision Hotel - Mji Mpya
47
0262320095
0784520192
23.
VETA Hotel
12
0756 698408
24.
Area D Lodge - Area D
8
0764 698408
25.
Formula One - Makole
8
0755 404621
26.
Summit Hotel - Ipagala
42
0715 816000
27.
Kitemba Hotel - Oneway
24
026 2323578
Wajumbe watalipwa posho ya kujikimu na watalazimika kujitegemea kwa gharama za malazi katika hoteli watakazofikia. 
1.0        USAJILI 
Zoezi la Usajili litafanyika kwenye Ofisi  ya Bunge Mjini Dodoma kuanzia Saa Tatu Asubuhi tarehe 16 Februari, 2014 hadi tarehe 17 Februari, 2014.
Zoezi hilo litajumuisha Ujazaji wa Fomu ya Usajili, Upigwaji Picha za Vitambulisho na Kukabidhiwa Begi lenye maelezo muhimu na stahiki nyinginezo kama zitakavyoainishwa.
Wajumbe wote wanapaswa kufika na nakala halisi ya vitambulisho vyao ili waweze kutambuliwa kwa usajili.
Vitambulisho vitakavyokubalika ni: -
(i)       Shahada ya Kupigia Kura;
(ii)      Kitambulisho cha Taifa;
(iii)    Kitambulisho cha Zanzibar;
(iv)    Hati ya Kusafiria;
(v)      Leseni ya Kuendeshea gari;
(vi)    Kitambulisho cha Mwajiri anayetambulika.
Iwapo Mjumbe hana kitambulisho chochote kilichoainishwa hapo juu basi anaombwa kuwasiliana na Maofisa waliotajwa katika Tangazo hili ili kuona namna anavyoweza kusaidiwa.
1.0        MKUTANO WA MAELEKEZO YA AWALI 
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu wa Baraza la Wawakilishi wameandaa Mkutano wa Maelekezo ya awali siku ya Jumatatu tarehe 17 Februari, 2014 kuanzia Saa Kumi Jioni.
  
Wajumbe wote wanapaswa kuhudhuria Mkutano huo bila kukosa ambao utajumuisha utaratibu wa ukaaji, jiografia ya viwanja vya Bunge na huduma za utawala.
1.0        SHUGHULI ZA KIKAO CHA KWANZA
Kikao cha Kwanza kitafanyika Siku ya Jumanne, tarehe 18 Februari, 2014 ambacho kitajumuisha Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda atakayesimamia upitishwaji wa Kanuni na Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
2.0        MAWASILIANO
Kwa taarifa zaidi, Wajumbe wanaombwa kuwasiliana na:
Ofisi ya Bunge Maalum,
S. L. P. 901,
DODOMA.
Simu:  026 23 22 696
Fax:    026 23 23 116
  
Aidha, Wajumbe wanaweza kupata ufafanuzi zaidi kutoka kwa Maafisa wafuatao:-
1.          Ndg. John Joel
(0754 260 831)
2.          Ndg. Amour Amour
(0777 855 878)
3.          Ndg. Kitolina Kippa
(0754 363 237)
4.          Ndg. Saidi Yakubu
(0762 089 225)
5.          Ndg. Abdu Haji
(0779 894 847)
6.          Ndg. Mossy Lukuvi
(0767 401 333)

 IMETOLEWA NA: 
OFISI YA KATIBU WA BUNGE NA KATIBU WA BARAZA LA WAWAKILISHI
            15 FEBRUARI, 2014   
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top