Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UMOJA WA MATAIFA WASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA UTAMADUNI MZURI WA KUENZI WANAWAKE WANAOLETA MABADILIKO KWENYE JAMII


DSC_0017
Pichani ni  Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet akizungumza na wanafunzi wa shule za sekondari mbalimbali za jijini Dar es Salaam na kuwaonyesha picha na kuwapa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ambayo wakinamama wamekuwa wakifanya kwa mustakabali kwa kuleta usawa na haki za wanawake duniani.


Shirika la Ufaransa la Alliance Francaise de Dar es Salaam liliandaa safari ya maonyesho iliyopewa jina “women in Resistance by the talented French photo-journalist Pierre-Yves Ginet.

Mwandishi wa habari huyo mpiga picha Pierre-Yves Ginet ambaye alifanya kazi ya kutafuta wanawake wanaojituma katika maisha yao ya kila siku na kazi zake zimeweza kuwapa ari na moyo wakinamama wengi Afrika.

Kati ya 2001 na 2006, alisafiri zaidi ya nchi 17 akipiga picha za wakinamama ambayo katika shughuli zao waliweza kufungua ukurasa mpya na kubadilisha historia katika kizazi cha leo.

Katika shughuli na katika njia tofauti walizotumia katika kubadilisha maisha wa wakinamama wengi duniani, wanawake kupitia kazi za picha Ginet wameweza kuwa na dhamira moja kubwa nayo ni kubadilisha maisha ili kuweza kuwa matumaini ya kuwa na maisha bora zaidi kwa sasa na baadaye.

Maonyesho hayo ya lengo la kuwapa usawa wakinamama wote kupitia mabara yote hapa duniani na hasa nchi zinazoendelea, sehemu za vita.
Na sehemu kubwa ya picha hizo zinaonyesha jinsi wakinamama wanavyopambana ili kujikwamua katika unyonge na ukandamizaji wa aina yoyote hapa duniani.
DSC_0025
DSC_0071
Mmoja wa wananfunzi akibadilishana mawazo na Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet anayetumia maonyesho ya picha mbalimbali kuelimisha jamii kupitia picha hizo.
DSC_0065
Afisa Habari kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo kwa wanafunzi wa shule za sekondari mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani.
Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani inayoambatana na siku ya Wanawake Duniani ni kufikisha sifuri katika kuondoa swala ukeketaji duniani.
Ujumbe unasema kwamba ukeketaji umepungua katika sehemu kubwa ya dunia na takwimu zinasema kwamba zaidi ya wanawake na wasichana 125 milioni ambao wanaishi katika dunia ya leo katika nchi 29 za Afrika na Mashariki ya kati walifanyiwa vitendo vya ukeketaji, na kama swala hii likiendelea zaidi ya wasichana 86 milioni duniani watafanyiwa vitendo vya ukeketaji kufikia mwaka 2030.
DSC_0102
Salome Anyoti kutoka shirika la umoja wa mataifa la wanawake akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa sekondari wa kutoka shule mbalimbali hapa Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kuangali picha za wakinamama walioleta mabadiliko katika maisha yao na wengine kwa ujumla.
DSC_0069
DSC_0030
Hizi ni baadhi ya picha za wanawake nchini Tanzania ambao wameleta mabadiliko katika maisha yao na wengine hapa nchini.
DSC_0028
DSC_0048
Baadhi ya picha zinazoonyesha matukio mbalimbali yaliyokusanywa na Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet.
DSC_0051

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top