Jeshi la polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu tisa wakiwemo wanawake wawili wa kijiji cha Mwabulimbu wilayani Maswa kwa tuhuma za mauaji ya kikatili ya kina mama wawili kuuawa na kuchomwa moto kwa kudaiwa kuzuia mvua kunyesha.
Mbali
na wanawake hao polisi pia inawashikilia viongozi wakuu wa jeshi la
ulinzi wa jadi “Sungusungu” akiwemo Mtemi na Kamanda wake mkuu kwa
tuhuma za mauji hayo ya kikatili kwa akina mama hao ambao baada ya
kushambuliwa sehemu mbalimbali za miili yao walichomwa moto kwa madai ya
kuzuia mvua kunyesha katika kijiji cha Mwabulimbu wilayani hapa.
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Simiyu Charles Mkumbo akiongea na waandishi wa
habari jana ofisini kwake alisema kuwa viongozi waliokamatwa ni Mtemi
mkuu wa sungusungu Ntalage Mabula (50) na Kamanda wake mkuu Sosoma
Mamuda (50) wote wakazi wa kijiji cha Mwabulimbu,kata ya Mwang’honoli
tarafa ya Sengerema wilayani Maswa mkoani hapa.
Wanawake
waliokamatwa kuhusiana na mauaji hayo ni Tabu Mongo (31) na Joyce Kija
(30) watuhumiwa wote ni wakazi wa kijiji cha Mwabulimbu kata ya
Mwang’honoli tarafa ya Sengerema wilayani Maswa.
Akielelezea
tukio hilo kamanda wa polisi alisema watuhumiwa wote walikamatwa
februari 4 kufuatia viongozi hao wakuu wa sungusungu mnamo februari pili
mwaka huu,kutoa amri na agizo la kupiga yowe na filimbi za hatari na
kukusanya wananchi waliowapiga na kuwaua na kuwachoma moto wanawake hao
wawili pia wakazi wa kijiji hicho.
Alisema
wananchi hao wakiwa na silaha zao za jadi,marungu,fimbo mawe waliwauwa
wanawake hao na kisha kuwachoma moto, waliofahamika kwa jina la Gilya
Chile (70) na Nyang’au Nyambalya (30) wote wakazi wa kijiji hicho.
Kamanda
Mkumbo alisema kuwa kabla ya mauaji hayo, kijiji hicho na maeneo
mengine wilayani Maswa na hata mkoa wa Simiyu yalikuwa yakikabiliwa na
ukame wa mvua kutonyesha, na inadaiwa kuwa akina mama hao waliomba
kuchangiwa gunia moja kila mmoja kwa vile wanatoka katika ukoo wa
kichifu ili mvua iweze kunyesha.
Kutokana
na kuwepo kwa hali hiyo Mtemi wa sungusungu kwa kushirikiana na Kamanda
wake mkuu wa Sunsungu Sosoma Mamuda (50) pia mkazi wa Mwabulimbu
walipiga yowe na filimbi za hatari kuhoji kulikoni akina mama hao kuzuia
mvua isinyesha kijijini hapo na ndipo walipoanza kuwaadhibu kwa
kuwashambulia kwa silaha za jadi.
Kamanda Mkumbo alieleza kuwa watuhumiwa wote hao watafikishwa mahakani mara baada ya upelelezi kumalizika.
Post a Comment