Jana mchana nilipita pale Kitanzini
nikamkuta Diwani Mteule wa Nduli ( CCM) Bashir Richard Mtove ( Mwenye
koti jeusi) kwenye mazungumzo na Katibu wa Chadema Mkoa wa Iringa ,
Allen Kilewella ( Kushoto kwake pichani) na wadau wengine wa siasa
kutoka CCM na Chadema. Nami nilijiunga kwenye mjadala, na hakika,
yaliyokuwa yakizungumzwa ni mambo ya msingi kuhusu changamoto za uongozi
na maendeleo. Kwamba wote ni Wana-Iringa, na kwamba kwenye mambo ya
msingi ni busara kujadiliana kindugu na kirafiki. Siasa si uadui.
Maggid,
Iringa.
Maggid,
Iringa.
Post a Comment