Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAMBO MAKUBWA ALIYOYAFANYA KATIBU MKUU WA CCM, ND KINANA AKIWA ZIARANI WILAYANI TEMEKE


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndungulile, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Temeke kwa ajili ya kuanza ziara katika wilaya hiyo leo ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku nne mkoani Dar es Salaam. Wapili ni Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu.
 Kinana akivishwa skavu baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Temeke
 Kinana akitoka katika ofisi ya CCM wilaya ya Temeke baada ya kuzungumza na Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo, Wapili ni Mtemvu na kulia ni Mkt CCM Dsm, Ramadhani Madabida
 Kinana na Madabida wakiwa katika bodaboda ya mwanachama wa VICOBA wakati Kinana, alipokuwa akienda kwenye mkutano wake na Vicoba Temeke katika ukumbi wa Kata ya 15 Pub, Temeke
 Mtemvu katika bodaboda wakati wa kwenda kwenye kikao hicho na Vicoba wa Temeke
 Kinana akishuka katika bodaboda baada ya kufika kwenye ukumbi wa Kata ya 15 Pub, kwenye mkutano na Vicoba Temeke. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam. Ramadhani Maadabiba.
 Kinana akiingia ukumbini na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke Yahya Sikunjema kwa ajili ya kuzungumza na Vicoba wa Temeke
 Vicoba wakimshangilia Kinana alipozungumza nao katika ukumbi wa Kata ya 15 Pub, Temeke
 Msanii wa Machozi Theatre Group, akionyesha machejo Kinana alipokutana na Vicoba, Temeke
 Mtemvu akimtuza msanii wa kikundi cha Machozi Theatre Group kikundi hicho kilipotumbuiza wakati Kinana kizungumza na Vicoba wa Temeke katika ukumbi wa Kata ya 15 Pub.
 Maliki Ndembo (65) akisoma gazeti la  Uhuru nje ya ukumbi wa Kata ya 15, Temeka
 Kinana akikagua mitambo ya mradi uliokuwa wa kusafisha gesi kutoka kwenye taka eneo la Mtoni, Temeke. Mradi wenye mitambo hiyo uliopo chini ya Jiji la Dar es Salaam, haukuwahi kufanya kazi hadi sasa na sasa Halmashauri ya wilaya ya Temeke inataka uwe chini ya miliki yake ili iweze kuundeleza.
Kinana akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick baada ya kukagua eneo la mradi huo.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana, Machi 26, mwaka huu, katika eneo la Kigamboni, wiulayani Temeke akiwa katika ziara yake mkoani Dar es Salaam, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua na kugagua utekelezaji wa ilani ya Chama. 
   Akizungumza na wananchi wa Kigamboni, Kinana ameahidi kulichukua suala linaloonekana kuzua mgogoro mkubwa baina ya wananchi na serikali la ujenzi wa mji wa kisasa wa Kigamboni, Kinana ameahidi kulifikisha kwenye vikao vya ngazi ya juu kabisa vya CCM kwa uamuzi wa uhakika na wa kudumu.
  Kinana amesema, baada ya kulifikisha kwenye vikao vya juu ya CCM atarejea tena Kigamboni kuzungumza na wananchi ili kuwapa majibu sahihi.
   "Hapa ni lazima tujue, wazo la kubuniwa mradi huu lilianzishwa na nani, kwa lengo na maslahi gani, na wananchi ninyi mnaoishi hapa mlihusishwa kwa kiwango gani kuhakikisha mchakato mzima unakuwa halali kwa mujibu wa sheria za nchi", alisema Kinana.
 
Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Kinana alipoowahurubia katia mkutano huo
 Kassim Abdallah mkazi wa Vijibweni Kigamboni akitoa hoja zake mbele ya Kinana kuhusu mradi huo
 Khalfan Iddi ambaye alikuwa kada wa CUF akikabidhi kadi yake kwa Kinana baada ya kuridhiwa na hotuba ya katibu mkuu huyo kwenye mkutano huo wa Kigamboni
 Kinana akiagana na wananchi baada ya mkutano
Kinana akiongdoka uwanjani baada ya mkutano. Kulia ni mwenyekiti wa CCM Temeke, Yahya Sikunjema. Picha zote na Bashir NKoromo wa CCM Blog
 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top