Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiweka mchanga katika kaburi la aliyekuwa Mkuu wa
Mkoa wa Mara, John Tupa, kwenye mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa
marehemu, Kilosa Machi 29, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa katika mazishi yaliyofanyika nyumbani
kwa Marehemu, Kilosa, Machi 29, 2014. (Picha na Ofifi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Mizengo Pinda akimfariji Mzee Gabriel Tupa baba mzazi wa
aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa katika mazishi yaliyofanyika
nyumbanikwa marehemu Kilosa achi 29, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
********
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa
wa Mara, John Tupa kwenye viwanja vya Nyerere mjini Dodoma Machi 28,
2014.Wengine pichani ni Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira a Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, William Lukuvi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda ameongoza viongozi mbalimbali na mamia ya wakazi wa
Mkoa wa Dodoma kuuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mara ambaye
alifariki dunia ghafla Machi 25, 2014 akiwa ziarani wilayani Tarime.
Shughuli
ya kuuaga rasmi mwili wa marehemu John Gabriel Tuppa kwa wakazi wa mji
wa Dodoma ilifanyika leo mchana (Ijumaa, Machi 28, 2014) kwenye viwanja
vya Mwalimu Nyerere ambako ibada ya kumwombea marehemu ilifanyika.
Baadaye mchana, mwili wake ulisafirishwa kwenda wilayani Kilosa, mkoani
Morogoro kwa mazishi.
Akizungumza
na waombolezaji hao kabla ya kutoa heshima za mwisho, Padri Chesco
Msaga ambaye aliongoza ibada hiyo, alisema Mungu aliwaumba wanadamu ili
wampende na wamtumikie na kwamba marehemu Tuppa alilitimiza jambo hilo
vilivyo.
Alisema
wakati wa uhai wake, Bw. Tuppa alipenda haki na popote alipokwenda
alitetea haki za wanyonge. “Sote ni mashahidi wa jinsi alivyopenda watu
na jinsi alivyowatumikia watu. Alikuwa mnyenyekevu, aliwasikiliza
wengine na alithamini michango ya wengine. Na sisi tunapaswa kuiga
hilo,” alisema.
Naye
Dk. Right Mmbaga, akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Baraza la
Wazee la Dodoma Mjini alisema: “Wale watumishi ambao bado wako kazini na
walipata nafasi ya kufanya kazi na Bw. Tuppa, wajifunze kutoka kwake na
wafuate nyayo zake kama njia ya kumuenzi.”
Naye
Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Mwigulu Nchemba, akitoa salamu kwa niaba ya
Katibu Mkuu wa CCM, alisema Chama cha Mapinduzi kimempoteza kamisaa
makini sana aliyekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya chama hicho.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), Bw. William Lukuvi
aliwaasa wakazi wa Dodoma kuenzi mambo ambayo Bw. Tuppa aliwafanyia
wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma hata kama walikuwa hawayaoni.
“Alikuwa
na upeo wa kufanya kazi kwa spidi lakini kwa utulivu. Wakati tumeanza
naye kazi hapa Dodoma mwaka 2006, kulikuwa na shule sita tu za sekondari
lakini katika kipindi cha miaka miwili alifanikisha kusimamia ujenzi wa
shule za sekondari 30,” alisema Bw. Lukuvi ambaye wakati huo alikuwa
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza
kwa niaba ya viongozi wa Makanisa ya mkoa wa Dodoma, Askofu Dk. Yohana
Masinga alisema viongozi hawajui kwamba wakishateuliwa, wao ni watumishi
wa Mungu kwa sababu wanawaongoza watu walioumbwa kwa sura na mfano wa
Mungu..
Akinukuu
neno la Mungu kutoka kitabu cha Waebrania sura ya 13 aya ya 7,
linalosema wakumbukeni waliokuwa wakiwaongoza, ichunguzeni miisho ya
mwenendo wao na iigeni imani yao, Askofu Masinga aliwataka wote waige
mfano wa utendaji kazi wa Bw. Tuppa.
“John
Tuppa alikuwa ni mtendaji na kanisa limempoteza mtu makini. Ninawaomba
viongozi wa nchi hii waige mfano wa John Tuppa. John Tuppa awe ni mfano
kwao, na wafanye hivyo kwa ukombozi wa nchi yetu,” alisema.
Bw.
Tuppa anatarajiwa kuzikwa kesho (Jumamosi, Machi 29, 2014) wilayani
Kilosa. Alizaliwa Januari mosi, 1950. Amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya za
Chunya, Mwanga, Bukoba, Muleba na Dodoma kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Mara mwaka 2011. Ameacha mke na watoto watano.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, MACHI 28, 2014
Post a Comment