Mwenyekiti
wa Wabunge wanawake Anna Abdallah (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa
Wabunge wanawake Dkt. Mary Mwanjelwa (kushoto) wakibadilishana mawazo
leo mjini Dodoma wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wanawake
wa Bunge la Katiba ili kujenga muafaka wa agenda muhimu kwa maswala ya
kijinsia.(Picha na Tiganya Vincent-Dodoma)
Makamu
Mwenyekiti wa Wabunge wanawake Suzan Lyimo akitoa mada leo mjini
Dodoma kwa wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba kuhusu uwakilishi
wa wanawake katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na umuhimu
wa kuwa kitu kimoja katika kujadilia masuala ya wanawake katika Bunge
Maalum la Katiba.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania(TGNP) Usu Mallya akitoa mada
leo mjini Dodoma kwa wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba kuhusu
uzingatiaji masuala ya haki za wanawake , utu na hali ya maisha na
mgawanyiko wa raslimali wakati wa uandishi wa Katiba mpya.
Mtoa
mada kutoka TAWLA Victoria Mandari akitoa mada leo mjini Dodoma kwa
wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba kuhusu umuhimu wa kuzingatia
masuala ya mirathi na ndoa katika uandishi wa Katiba mpya.
Baadhi
ya wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia mada
mbalimbali wakati wa semina ya kuwajengea uwezo ili wasaidie kutetea
kuingizwa kwa vifungu mbalimbali katika Katiba inayotarajiwa kuandika
vinavyopinga unyanyasaji wa kijinisia.
Post a Comment