Klabu ya Simba itafanya mkutano wa wanachama wake Jumapili (Machi 16 mwaka huu) kwa ajili ya kuifanyia marekebisho Katiba yao.
Nachukua
fursa hii kuwatakia kila la kheri katika mkutano huo ambao ni muhimu
katika kuhakikisha klabu yao inapiga hatua katika maendeleo ya mpira wa
miguu na ustawi wake kwa ujumla.
Hata
hivyo, nawakumbusha viongozi na wanachama wa klabu ya Simba kuwa
marekebisho hayo ni lazima yafanyike kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na
maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Afrika
(CAF) na Tanzania (TFF).
credit: www.bkmtata.blogspot.com
Post a Comment