Afisa
Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Viwanda na Biashara Nicodemus Mushi,
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukaguzi wa leseni za biashara
kwenye ukumbi wa MAELEZO leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Uhamasishaji wa Masoko wa waizara hiyo Christopher
Mashingo.Kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari (MAELEZO), Frank
Mvungi.Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Uhamasishaji wa Masoko wa waizara hiyo Christopher
Mashingo.Kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari (MAELEZO), Frank Mvungi.
Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
Waandishi
wa Habari wakiwa kazini kwenye mkutano kati ya wawakilishi wa Wizara ya
Viwanda na Biashara (hawapo pichani) na waandishi hao, kwenye ukumbi wa
Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam leo. Picha na Hussein
Makame-MAELEZO.
…………………………………..
Hussein Makame-MAELEZO
WIZARA
ya Viwanda na Biashara imewataka wananchi kufuata sheria na taratiu za
nchi katika kuendesha biashara zao kwani kufanya hivyo ni alama ya
maendeleo na kigezo kimoja cha kupima maendeleo ya watu ni jinsi
anavyofuata taratibu.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uhamasishaji wa Masoko wa
wizara hiyo, Christopher Mashingo wakati akizungumza na waandishi wa
habari ukaguzi wa leseni za biashara leo jijini Dar es Salaam.
Mashingo
alisema Serikali ilirejesha utaratibu wa kupata leseni ya biashara kwa
kulipia kuanzia Julai 1 mwaka jana na kutoa kipindi cha miezi 6 kwa
wafanyabiashara waliokuwa na leseni zisizo na ukomo kuhuisha leseni zao.
Alisema
kipindi hicho kiliisha Desemba 31 mwaka na wale waliochelewa kufanya
hivyo walipata leseni zao kwa kulipa ada na adhabu kwa mujibu wa Sheria
ya Leseni Namba 25 ya mwaka 1972 kifungu cha 11 (a) na (b).
“Wito
kwa wananchi kufuata kufuata sheria na taratiu za nchi katika kuendesha
biashara zao kwani kufanya hivyo ni alama ya maendeleo na kigezo
kimoja cha kupima maendeleo ya watu ni jinsi anavyofuata taratibu”,
alisema Mashindo.
Alisema
ofisi yake inafanya ukaguzi ili kuhakikisha kuwa biashara zinafanyika
kwa mujibu wa Sheria na Taratibu za nchi kama alivyoagiza Katibu Mkuu wa
Viwanda na Biashara.
Aliongeza
kuwa Katibu Mkuu huyo aliagiza kwamba Mamlaka za Leseni zifanye ukaguzi
wa kina katika maeneo yao, na kusisitiza kuwa ukaguzi huo ufanyike kati
ya mwezi April na Mei.
Post a Comment