Na Mwandishi Wetu, Dar
MSHAMBULIAJI
na mpachika mabao wa Yanga na Nahodha wa timu ya Taifa ya Burundi,
Didier Kavumbangu, leo mchana amesaini Mkataba wa miaka miwili na
mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC.
Kavumbangu
aliyemaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC, ameamua kusaini Azam
FC baada ya kuona Klabu yake haina mawasiliano naye licha ya kumaliza
Mkataba wake.
“Mimi ni mchezaji, kazi yangu
ni mpira. Nimemaliza mkataba Yanga, lakini viongozi hawaniambii kitu,
nimepata ofa nzuri Azam nikaamua kusaini,” amesema
Akizungumza na Mwandishi wa
habari hizi, Kavumbangu, baada ya kusaini Mkataba huo ambao unamfanya
alipwe vizuri kuliko alivyokuwa analipwa Jangwani.
Pamoja
na hayo, Kavumbangu ameishukuru Yanga SC na mashabiki kwa miaka miwili
aliyoichezea timu hiyo na anasema itabakia kwenye kumbukumbu zake kwa
kushinda nayo mataji kadhaa.
Mshambuliaji
huyo mrefu mwenye nguvu amesema sasa akili yake anaipeleka kwa mwajiri
wake mpya, Azam FC ambako pia amepania kwenda kushinda mataji na
kuiwezesha timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na
familia yake kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika.
“Mimi sasa ni mchezaji wa Azam,
nafurahi kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida yangu huwa nashabikia
klabu nayochezea, sasa mimi ni mshabiki namba moja wa Azam,”amesema.
Kavumbangu
alitua Yanga mwaka 2012 akitokea Atletico ya Burundi na katika mechi
misimu miwili ya kuichezea klabu hiyo, amefunga mabao 31 katika mechi 63
za mashindano yote, moja tu la penalti.
Post a Comment