Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LIVERPOOL RAHA MPAKA BASI, PENALTI MBILI ZA GERARD ZAFANYA KILELENI YAWE MAKAZI YAO YA KUDUMU

 






Haijalishi, sisi ubingwa tu: Steven Gerrard akisherehekea na wenzake baada ya kufunga penalti iliyoipa bao la ushindi Liverpool
 
****************

MABAO mawili ya penalti ya Steven Gerrard yameipa ushindi wa 2-1 Liverpool na kuweka hai matumaini ya ubingwa wa Ligi Kuu ya England.


Lakini timu zote, West Ham na Liverpool ziliondoka uwanjani zimemkasirikia refa Anthony Taylor kwa kuvurnda katika maamuzi yake kwenye mchezo huo ambayo yaliiponza timu kufungwa bao.

West Ham walilalaimia penalti iliyotolewa kabla ya mapumziko baada ya James Tomkins kuunawa mpira na Gerrard akafunga dakika ya 44. Lakini wachezani wa Liverpool walilalamikia pia bao la kusawazisha la West Ham lililofungwa Guy Demel dakika ya 45.

Mshambuliaji wa zamani wa Wekundu hao wa Anfiled, Andy Carroll alimchezea rafu ya wazi na kipa Simon Mignolet wakati wa mpira wa kona, akimpiga kichwani na kusababisha Mbelgiji huyo mpira umponyoke na kuangukia kwa Guy Demel, aliyefunga akiwa anatazamana na nyavu.

Liverpool ilipata bao la pili kwa penalti ya utata, baada ya kipa wa West Ham, Adrian kudaiwa amemchezea rafu Jon Flanagan, lakini picha za marudio ya Televisheni zilimuonyesha mlinda mlando huyo akiufikia mpira kwanza na Gerrard akaenda kufunga.

Ushindi huo unaifanya Liverpool ifikishe pointi 74 baada ya kucheza mechi 33 na kuendelea kula raha kileleni mwa Ligi Kuu ya England, mbele ya Chelsea yenye pointi 72 za mechi 33 na Manchester City yenye pointi 70 za mechi 31.


Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top