Cristiano
Ronaldo aliifungia ureno bao la ushindi timu yake ilipoilaza Black
Stars ya Ghana 2-1 katika mechi ya mwisho ya makundi.
Kinaya ni kuwa Ureno ilikuwa keshabanduliwa nje ya kipute hicho baada ya kushindwa mechi zao za kwanza.
Ghana
itajilaumu yenyewe kwa kushindwa kusajili ushindi uliohitajika
kuihakikishia nafasi katika 16 bora baada ya John Boye alipojifunga
mwenyewe.
Asamoah
Gyan alifunga bao la kuisawazishia Black stars lakini haikutosha
kuifufua kampeini yao kwani walihitaji ushindi wa aina yeyote na kuomba
kuwa Ujerumani ishinde marekani iliwaweze kufuzu kama washindi wa pili
katika kundi G.
Ronaldo
hata hivyo atamshukuru kipa wa Ghana Fatawu Dauda kwa sifa alizopata
baada ya kufunga bao la ushindi kufuatia kipa huyo kumzawadia mpira
katika eneo la lango naye akaifuma kimiani.
Kufuatia ushindi huo wa ureno Ghana ilikamilisha mechi za makundi ikiwa na alama moja pekee huku ureno ikiwa ya tatu na alama 4.
Marekani walijiunga na ujerumani katika mkondo wa pili licha ya Ujerumani kuibana marekani kwa bao moja bila ya jibu.
Ghana
hata hivyo ilikuwa tayari inakumbwa na kashfa ambayo wachezaji wake wa
kutegemewa Kevin Prince Boateng na Sulle Muntari walitimuliwa kambini
huku wale waliosalia wakitishia kususia mechi hiyo ya Ureno kufuatia
ubishi kuhusiana na malimbikizi ya marupurupu yao.
Post a Comment