Na Ismail Ngayonga, MAELEZO
SERIKALI
ya Jamhuri ya Watu imeikabidhi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
msaada wa gari la kurushia Matangazo lenye thamani ya Tsh. Bilioni 6 ili
kuboresha utendaji wa shughuli za shirika hilo.
Akipokea
msaada huo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara alisema msaada ni kielelezo
cha urafiki wa kweli wa kimaendeleo katika nyanja mbalimbali uliopo
baina ya Tanzania na China.
Mukangara
alisema gari hilo litaisaidia TBC kuteleza majukumu yake kikamilifu na
hasa katika kipindi hiki ambacho matangazo mengi ya Televisheni yamekuwa
yakirushwa katika mgumo wa dijitali. “Tupo katika mradi kwa
kushirikiana na STARTIMES kuhakikisha kuwa TBC inafika katika kona zote
za Tanzania na kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi” alisema Waziri
Mukangara.
Kwa
mujibu wa Waziri Mukangara alisema Mwezi Oktoba mwaka huu (2014) Rais
Jakaya Kikwete atafanya ziara ya kikazi nchini China ambapo pamoja na
mambo mengine, Serikali ya China imepanga kuipatia Tanzania mkopo wa
liba nafuu ambao utasaidia TBC kujipanga na kufikia malengo yake kwa
muda mfupi.
Aidha
Waziri Mukangara alisema upo umuhimu mkubwa wa kuimarisha uhusiano wa
vyombo vya habari baina ya Tanzania na China kwani kutasaidia
kubadilishana utamaduni baina ya nchi hizo mbili. “Kupitia Matangazo ya
televisheni tutaweza kubadilisha fikra za jamii zetu na TBC ni lazima
iweze kuwa imara katika Nyanja zote” alisema Waziri Mukangara.
Kwa
upande wake Mkurungezi Mkuu wa TBC, Clement Mshana alisema msaada huo
umekuja katika wakati mwafaka kwani lengo la TBC kwa sasa imejipanga
kikamilifu sekta ya michezo ikiwemo mpango wa kuonyesha matangazo ya
moja kwa moja kutoka katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa
lengo la kuonyesha ulimwengu vipaji vya wanamichezo vilivyopo Tanzania
wachezaji waliopo Tanzania.
“Uwanja
wa Taifa kwa sasa umekamilifu kwa kiasi kikubwa na hasa katika eneo la
mchezo wa mpira wa Miguu, na sisi tumejipanga kuonyesha michezo yote ya
mpira wa miguu kuanzia mechi za ndani hadi nje ya nchi’ alisema Mshana.
Post a Comment