Kocha mpya wa klabu ya Yanga Marcio Maximo. |
Aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya hapa nchini Maxio Maximo kutoka
Brazil amepata fursa ya kurudi tena hapa nchini, kuja kuisuka vyema timu
ya Yanga ili iweze kucheza katika michuano ya kimataifa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye makao makuu ya klabu ya
Yanga, Jangwani, wakala aliyemleta Maximo, Ally Mlee alisema kuwa,
ilimchukua miaka 3 kumuomba kuja hapa nchini kusuka timu ya yanga, kwa
kujali kwake na ukarimu wa watanzania amekuja tena hapa nchini na
amesaini mkataba wa miaka miwili.
Kwa upande wake Maximo alisema kuwa, amefurahi kuja kusuka timu ya
yanga na anamatumaini itafanya vyema katika michuano mikubwa nje ya nchi
lakini hata katika ligi ya hapa nyumbani.
“Watanzania ni wakarimu sana ndio maana nimekubali kuja tena hapa
nchini kuinoa Yanga, lakini pia ujio wangu nimekuja na kocha msaidizi
ambaye atanisaidia kusimamia na pia nitapendekeza wachezaji wazuri
kutoka katika timu kubwa huko Ulaya, ili waje kuchezea Yanga lakini pia
ni fursa kwa wachezaji wa yanga kujinoa kupitia wachezaji wakubwa,”
alisema Maximo.
Siku ya Jumatatu timu ya Yanga itaanza mazoezi na mwalimu huyo mpya, maandalizi ya kujiandaa na ligi mbalimbali.
Post a Comment