Mkali wa Sound Track ambaye pia ni mkali wa kuvunja (dancer)
amezungumzia uhusiano wake na muigizaji mrembo wa Bongo Movies, Irene
Uwoya.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Msami alizunguka sana mbuyu
kutaka kutoa maelezo kuhusu ukweli wa mambo kati ya wawili hao lakini
kwa mara ya kwanza aliamua kuiambia tovuti ya Times Fm kauli yake kutokana na jinsi alivyoulizwa.
“Kaongea kwa upole huyu jamaa, kaapproach ili apate jibu. Ni
kweli (kicheko)…nimekuridhisha lakini, nimeamua kukuridhisha.” Amesema
Msami..
Muonekano wa Irene Uwoya na Msami kwa muonekano uliwafanya wengi
wazungumze kwenye mitandao ya kijamii kuwa Msami amegeuka Serengeti Boy
kwa Uwoya ambaye wanaamini anamzidi sana umri. Lakini ukweli ni kwamba
Msami ni mkubwa kwa Uwoya. Chukua hiyo!
“Unajua mimi mwanzo, Serengeti Boy nilikuwa sina tafsiri yake
kabisa yaani. Yaani ile deeply nilikuwa sina tafsiri yake kabisa yaani.
Kwa hiyo leo ndio nimepata tafsiri yake ‘Serengeti Boy’ kumbe ni mtu
ambaye amezidiwa umri. Tofauti na mimi nilivyokuwa nawaza kuhusu
Serengeti Boy.
“Lakini mbona nikasema kama ni hivyo, as we are best friends
lakini (joke), lakini mbona mimi nimemzidi umri Uwoya. Lakini mimi ni
mkubwa kwake sema yeye ananizidi umri. Mimi ni mkubwa kwake nimemzidi
miezi mingi…yaani wewe jua nimemzidi miezi mingi. Mimi ni mkubwa kwa
Uwoya.” Alisisitiza Msami
Katika hatua nyingine, Msami ameeleza mpango wake na Uwoya kutoa filamu ya pamoja na jinsi filamu itakavyokuwa.
Amesema katika filamu hiyo yeye ndiye mhusika kuu na kwamba ni
filamu ambayo itahusisha dance na muziki. Filamu hiyo itatoka mwaka huu
lakini bado haijapata jina rasmi na tarehe ya kutoka.
“Movie inakuja very soon, watu wakae tayari.” Amesisitiza.
Post a Comment