Rais wa Simba SC, Evans Aveva (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari
|
RAIS
mpya wa Simba SC amemteua Zacharia Hans Poppe kuendelea kuwa Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, huku Makamu wake akiwa ni Kassim
Mohammed Dewji.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mchana wa leo makao makuu ya klabu, Msimbazi,
Dar es Salaam Aveva aliwataja Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa ni Said Tuliy,
Musley Al Ruwaih, Crescentius Magori na Dk Roadney Chiduo
Aveva
pia ameunda Kamati mbili zaidi, ya Soka ya Vijana itakayokuwa chini ya
Mwenyekiti, Said Tuliy, Ally Suru, Patrick Rweyemamu, Mulamu Nghambi,
Madaraka Suleiman na Amina Poyo.
Kamati
ya Mashindano Mwenyekiti wake atakuwa Mohammed Nassor, Makamu Iddi
Kajuna na Wajumbe Jerry Yambi, Hussein Simba na Mohammed Omar.
Aveva amesema pia
baada ya kikao cha kwanza cha Kamati ya Utendaji jana, Mohammed Nassor,
Musleh Al Ruwaih na Salim Abdallah wameteuliwa katika Kamati ya
Utendaji.
Aveva
amesema kikao cha jana pia kiliamua kuwasimamisha uanachama, wanachama
69 waliokwenda Mahakamani kupinga uchaguzi wa klabu hiyo mwishoni mwa
mwezi uliopita.
Amesema
hatima ya wanachama hao, pamoja na ya mwanachama mwingine maarufu,
Michael Wambura aliyeenguliwa kwenye uchaguzi kwa kosa kama hilo,
itaamuliwa katika Mkutano Mkuu Agosti 3, mwaka huu.
Post a Comment