Mahmoud Ahmad -Arusha
Zaidi
ya washiriki 56 wanashiriki katika Kongamano la kujadili sekta ya
uziduaji na uchanjuaji wa sekta ya madini mafuta na gesi katika sekta za
sheria,kanuni,sera na mikataba kwa watendaji wa sekta hiyo kutoka
kwenye nchi za jumuiya ya Afrika mashariki.
Akizungumza
na vyombo vya habari mkuu wa kitengo cha madini kanda ya
kaskazini(TMG) Mhandisi Gilay Shamika alisema kuwa kongamano hilo la
siku mbili lilovuta wadau wa sekta ya madini kutoka nchi za Kenya Uganda
na wenyeji Tanzania na kuandaliwa na taasisi ya Global Academy ya
nchini Uingereza.
Shamika
alisema kuwa sekta ya madini na gesi imekuwa na changamoto mbali mbali
ambazo zinahitaji elimu na ufahamu wa hali ya juu kwenye Nyanja hiyo
hivyo wanakutana kujadiliana kwa pamoja na wenzao kuweza kupata uelewa
zaidi.
Aidha
alisema kuwa wadau hao kutoka sekta za sheria,madini na fedha ndiyo
wanahusika katika kongamano hilo huku wakipata uelewa ni jinsi gani
watakavyoweza kuongeza kiwango cha uchangiaji wa pato la taifa kutokana
sekta ya madini hususani Mafuta na Gesi.
Giley
alisema kuwa sekta ya madini hususani kwenye eneo la Mafuta na gesi
limekuwa na changamoto mbali mbali hivyo ni sekta muhimu kuielewa kwa
mapana hivyo wao na taasisi hiyo wanajadili kuweza kuzinufaisha nchi za
ukanda huu.
Post a Comment