Mwanamume
wa Ujerumani ambaye anaongoza rikodi ya dunia kuwa na mwili uliotogwa
mara nyingi kabisa ameketaliwa ruhusa ya kuingia Dubai, baada ya kwenda
huko kutokeza katika klabu ya starehe.
Rolf Buchholz, ametogwa mwahala 453 kwenye mwili na uso wake na ana pembe mbili kwenye kipaji.
Ameeleza
kwenye mitandao ya kijamii kuwa alikataliwa na maafisa wa uwanja wa
ndege kuingia nchini kwa sababu, kama alivosema, alikuwa "mchawi".
Bwana Buchholz ameapa kuwa hatarudi tena Falme za Kiarabu.Chanzo BBC Swahili
Post a Comment