Sanamu: Phil Neville amsema Wayne Rooney anaweza kufanikiwa kujengewa sanamu kama ataendelea kufanya makubwa.
PHIL
Neville amedai kuwa Wayne Rooney anaweza kuwa gwiji wa Manchester
United na hata kupata heshima ya kujengewa sanamu katika klabu hiyo.
Beki
huyo wa zamani wa United aliyasema hayo wakati anazungumzia nahodha
mpya wa klabu na alidai kama mchezaji huyo wa zamani wa Everton anataka,
anaweza kuingia katika orodha ya wachezaji wakubwa zaidi waliowahi
kutokea katika historia ya klabu.
“Kama
unavunja rekodi ya Bobby Charlton katika klabu ya Manchester United,
unazungumzia heshima ya sanamu,” Neville aliwaambia The Mirror.
“Kwasababu
amekuwa mchezaji mkubwa kwa wakati wote. Watu wanampenda Wayne Rooney,
ninaposema anastahili sanamu, namaanisha kuwa ni mchezaji mkubwa.
Post a Comment