Baadhi
ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour
lililofanyika mkoani Dodoma jana,leo walipitia nyumbani kwa Mfalme wa
Rhymes a.k.a Simba Mzee a.k.a Afande Sele kumpa mkono wa pole na
kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea
mwisho mwa wiki mjini Morogoro.Pichani ni Msanii wa Muziki wa Bongofleva
atambulikae kwa jina la Shilole akimfariji Afande Sele
Malkia
wa Taarab hapa nchini,Bi Khadija Kopa akimfariji Afande Sele,pichani
nyuma ya Afande Sele ni guli wa muziki wa Reggae hapa nchini ,Innocent
Nganyagwa.
Afande Sele akifarijiwa na mkali wa hip hop katika anga ya muziki wa Bongofleva,Joh Makini
Baadhi ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour
lililofanyika mkoani Dodoma jana,wakiwa katika picha ya pamoja na Afande
Sele mara baada kupitia nyumbani kwa msanii huyo na kumpa mkono wa pole
na
kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea
mwisho mwa wiki mjini Morogoro.
Pichani
ni mmoja Wanahabari kutoka gazeti la Mwananchi na Efm,Henry Mdimu,Joh
Makini pamoja na Ben Paul wakiwa katika picha ya pamoja.
Wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kumfariji Afande Sele.Picha zote
kwa hisani ya Dj Choka aliyekuwepo kwenye msafara huo,Afande Sele
aliwashukuru Marafiki,washabiki wake ndugu jamaa na Marafiki kwa umoja
na mshikamano waliouonesha kwake katika kipindi hiki kigumu ambacho
hakikuwahi kumtokea katika maisha yake ya kuondokewa na Mpendwa
Mke/mzazi mwenzake. '' sina maneno yanayoweza kuelezea kwa wepesi
faraja,upendo na ushirikiano nilioupata kutoka kwenu,nawashukuruni sana
ndugu zangu'' ,alimaliza kusema Afande Sele huku akionekana kuwa mwenye
simanzi kubwa
Post a Comment