Mkurugenzi
wa Tan Communication Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye
makao yake makuu jijini Arusha Bw Robert Francis akiwa katika picha ya
pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kufanya halfa fupi
iliyofanyika mjengoni kwao ,ya kuwapongeza kwa kushika nafasi ya kwanza
katika sekta ya mawasiliano na habari kwa ukanda wa kaskazini maonyesho
ya nane nane, Pamoja na David Rwenyagira aliyepata Tuzo za Tanapa hivi karibuni
Mkurugenzi
wa Tan Communication Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye
makao yake makuu jijini Arusha Bw Robert Francis akiwa anampongeza
Mfanyakazi wa kituo hicho David Rwenyagira
kwa kupata Tuzo na kushika nafasi ya kwanza upande wa Redio katika eneo
la kutangaza utalii wa ndani na mshindi wa pili pekee kundi la
kutangaza masuala ya Uhifadhi upande wa Redio zilizotolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) hivi karibuni.
David Rwenyagira
akiwa anatoa pongezi kwa Mkurugenzi wao kwa kuweza kuona mchango wao
katika kampuni hiyo ambapo pia aliwataka wamiliki wa vyombo vya habari
hapa Nchini kutoa ushirikiano kwa wanahabari wao katika kuibua habari
za kijamii ikiwa nipamoja na kuwaezesha kufika vijijini
Bw
Robert Francis akiongea na wafanyakazi wa kampuni hiyo, ambapo pia
alitumia fursa hiyo kuvitaka vyombo vya habari kuandika na kutangaza
habari zinazohusu wakulima vijijini hali itakayosaidia kupatikana kwa
wataalam wa kuwasaidia katika kilimo ikiwa nikukuza ajira katika upande
wa kilimo
Pia amewaomba waandishi wa habari
Tanzania kupeleka kazi zao katika mashindano mbalimbali hali
itakayosaidia kujipima na kuongeza ujuzi zaidia huku akimtolea mfano
mtangazaji wa kituo hicho David Rwenyagira
aliyepata TUZO na kushika nafasi ya kwanza upande wa Redio katika eneo
la kutangaza utalii wa ndani na mshindi wa pili pekee kundi la kutangaza
masuala ya Uhifadhi upande wa Redio zilizotolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) hivi karibuni
Watangazaji wa kituo hicho wakiwa katika halfa
Ulaji ulikuwa hivi..
Mtangazaji Clara Moita akiwa anajipakulia katika halfa
Semio Sonyo wa kipindi cha Love cuts akiwa anafanya yake
Wafanyakazi wakiwa katika nyuso za furaha baada ya halfa
( Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Post a Comment