Majaji
wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakifuatilia Filamu fupi
iliyochezwa na baadhi ya washiriki wa Shindano la Tanzania Movie talents
(TMT) wakati ilipokua ikionyeshwa kwenye runinga kubwa katika Ukumbi wa
Makumbusho. Kutoka Kulia ni Single Mtambalike au Rich Rich katikati ni
Vyonne Cherry au Monalisa na Kushoto ni Jaji Mkuu wa Shindano hilo Roy
Sarungi.
Mahosti
wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwajibika
katika Jukwaa la Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wakati shindano hilo
lilipokuwa likiendelea alhamisi iliyopita.
Mmoja
kati ya Washindi kutoka Kanda ya Pwani, Mkoa wa Dar Es Salaam katika
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Shiraz Ngassa (wa Kwanza
Kushoto) akiongea na Msanii Joti mara baada ya Kuaga rasmi shindano hilo
lililofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa siku ya alhamisi.
Fredy
Kiluswa ambae pia alikuwa mmoja kati ya Washindi watano kutoka Kanda ya
Pwani katika Hatua ya kuwatafuta washindi wa Kanda akitoa maneno ya
Shukrani mara baada ya kuaga shindano hilo kutokana na uchache wa kura
alizopata.
Baadhi
ya washiriki wa kundi la Kwanza wakiwa mbele ya Majaji wa Shindano la
Tanzania Movie Talents (TMT) mara baada ya Filamu yao fupi kuonyeshwa.
Mwinshehe
Mohamed ambae alikua mmoja kati ya Washindi wa Tatu kutoka Kanda ya
Kati mkoa wa Dodoma akitoa pongezi na Maneno ya Shukrani kwa Timu nzima
ya TMT mara baada ya kuaga shindano alhamisi katika Ukumbi wa Makumbusho
ya Taifa.
Baadhi
ya washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) waliofanikiwa
kuingia hatua ya Fainali ambapo mshindi wa Shindano hilo linalotarajiwa
kufikia Tamati Mnamo mwisho wa Mwezi wa Nane kwa Mshindi Kukabidhiwa
Kitita Cha Shilingi Milioni hamsini za Kitanzani.Picha Zote na Josephat
Lukaza - Proin Promotions ltd
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Hatimaye
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limefikia hatua ya Mwisho
kabisa mara baada ya washiriki kumi bora kupatikana katika Show ya
Mchujo iliyofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa siku ya
Alhamisi.
Show
hiyo ya Mwisho katika katika Hatua ya mchujo ilifanyika siku ya Alhamisi
na kupelekea Washiriki watatu kutoka Kanda Mbili za Tanzania yaani
Kanda ya Kati na Kanda ya Pwani kuondolewa katika Kinyanganyiro hiko na
Kupelekea Shindano hilo kubaki na washiriki 10 tu ambao wameingia hatua
ya fainali ambapo mshindi mmoja ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni
50 za kitanzania katika Fainali Kubwa inayotarajiwa kufanyika katika
Ukumbi wa Mlimani City siku ya Tarehe 30 Mwezi huu wa Nane.
Washiriki
waliondolewa katika Kinyanganyiro Hiko ni Mwinshehe Mohamed ambae
alikuwa mmoja kati ya Washindi watatu kutoka Kanda ya Kati ambapo
anafanya Idadi ya washiriki wawili kutoka Kanda ya Kati kuondolewa na
Kuifanya Kanda ya Kati kuwakilishwa na Mshindi Mmoja katika Fainali
hiyo. Wengine waliotoka ni Shiraz Ngassa na Fredy Kiluswa ambao wote ni
Washindi kutoka kanda ya Pwani Mkoa wa Dar Es Salaam. Kanda ya Pwani
walichukuliwa washindi watano huku Shiraz na Fredy wakitimiza idadi ya
Washiriki wanne kuondolewa katika kinyanganyiro hiko kwa Kanda ya Pwani,
Tishi Abdallah ndie Mshindi mmoja kati ya washindi watano kutoka kanda
ya Pwani ambae anaiwakilisha Kanda ya Pwani katika Fainali kubwa ya
Shindao la Kwanza na la Kipekee kufanyika Afrika Mashariki na Kati la
Tanzania Movie Talents (TMT).
Mpaka
Sasa Ni Kanda Moja tu ambayo washindi wake wote watatu ndio
wanaiwakilisha Kanda hiyo katika Fainali kubwa itakayofanyika Mwishoni
Mwa Mwezi wa Nane katika Ukumbi wa Mlimani city ambapo mshindi mmoja
ataondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania huku washindi
wote kumi waliofanikiwa kuingia Katika hatua ya Fainali watakuwa chini
ya Kampuni ya Proin Promotions limited ambapo watacheza filamu ya pamoja
na Hatimaye kuanza kunufaika na Mauzo ya Filamu hiyo inayotarajiwa
kutoka Hivi Karibu.
Vipindi
vya Shindano hili la Tanzania Movie Talents (TMT) vitaendelea kurushwa
katika Kituo cha Runinga cha ITV siku ya Jumamosi Saa 4 Usiku huku
marudio yake yakiwa siku ya Jumapili Saa 10 Jioni na Siku ya Jumatano
saa 5 usiku.
Ili
Kuendelea kumuwezesha Mshiriki wako kuibuka mshindi wa Shindano la
Tanzania Movie Talents (TMT) kwa Mwaka 2014 unachotakiwa ni kuendelea
kumpigia kura kwa wingi kadri uwezavyo kwa Kuandika Ujumbe Mfupi wa
Maneno (SMS) Neno TMT acha nafasi ikifuatiwa na namba ya Mshiriki halafu
tuma kwenda 15678. Mfano TMT 00 halafu tuma kwenda 15678 au unaweza kupiga kura pia kupitia Ukurasa wetu wa Facebook kwa kufungua kiunganishi hiki https://www.facebook.com/tztmt/app_316963748468949
credit: Lukaza blog
Post a Comment