Ajali
nyingine mbaya:Basi la Abiria linalofanya safari zake kati ya Dar es
Salaam - Tabora limepata ajali mbaya sana mchana huu katika eneo la
Kiegeya,Gairo na kupelekea zaidi ya watu wanne kupoteza maisha huku
wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana.Ni majonzi makubwa yametawala
katika eneo hilo hivi sasa,huku juhudi za kuokoa miili na majeruhi
zikiendelea kama inavyoonekana pichani.ni siku tatu tu zimepita toka
ajali nyingine mbaya itokee huko Musoma na kupoteza maisha ya zaidi ya
Watanzania 35.Ripota wa Globu ya jamii yupo eneo la tukio hivi sasa na
taarifa kamili itawajia baadae kidogo.
Loading...
Home » Unlabelled » ajali nyingine mbaya yatokea Gairo mchana huu,zaidi ya watu wanne wanasadikiwa kupoteza maisha
Post a Comment