Naibu
Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles
Tizeba akipanda boti kuelekea kisiwa cha Nyamango kulikotokea ajali ya
moto kwa ajili ya kukabidhi misaada.
Na Daniel Makaka, Sengerema
NAIBU
Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Buchosa Dk Charles
Tizeba ametoa msaada kwa wahanga wa ajali ya moto na nyumba
zilizoezuliwa na mvua ya upepo katika kisiwa cha Nyamango kijiji cha
Lushamba kata ya Bulyaheke jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoa wa
Mwanza.
Misaada
aliyoitoa kwa wahanga hao ni Blanketi mia tatu na Magunia manne ya Unga
wa Mahindi na moja la Maharagwe vyote vyenye thamani ya shilingi
million tatu na laki tano ambavyo vimetolewa kwa kaya hamsini na moja
ambazo zilikumbwa na janga hilo Septemba 19 na 20 mwaka huu.
Akikabidhi
misaada hiyo Dk Tizeba aliwataka viongozi kuhakikisha misaada hiyo
inawafikia walengwa na siyo vinginevyo lakini pia aliwaasa wahanga hao
hao kutumia misaada kwa lengo la kuwasaidia wakati kamati ya maafa
wilaya ya Sengerema ikiwa bado inaendelea kufanya tathimini il iione
namna ya kuwasaidia.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles
Tizeba akiwa ndani ya boti kuelekea kukabidhi misaada katika kisiwa cha
Nyamango jimboni kwake.
…..Serikali itaendelea kusaidia kadri iwezavyo si kwamba watapewa fidia bali ni misaada tu.
Awali
Katibu wa kamati ya maafa wilaya Sengerema Bw. Benard Myatilo akitoa
taarifa ya wahanga wa tukio hilo alisema kuwa matukio hayo yalitokea kwa
nyakati tofauti ambapo Septemba 19 majira ya saa nane usiku kaya 40
ziliteketea kwa moto na chanzo cha moto huo ni kulipuka kwa Kibatari
ndani ya nyumba na tukio la pili kaya 11 kuezuliwa na mvua ilyoambatana
na upepo likiwemo jengo la kanisa Katoliki kisiwani humo.
Pia
alisema kati ya wahanga hao hakuna mtu aliyejeruhiwa katika matukio hayo
licha mali zote zlizokuwemo kuteketea ambapo hadi sasa kaya saba hazina
mahali pakuishi huku zilizobaki zikihifadhiwa na baadhi ndugu na jamaa
wanaoishi katika kisiwa hicho.
Muonekano wa baadhi ya nyumba zilizoteketea kwa moto katika kisiwa cha Nyamango wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.
Kanisa la Roman Katoliki katika kisiwa cha Nyamango lililoezuliwa na upepo ulioambatana na mvua.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles
Tizeba (mwenye suti ya kijivu) akikabidhi misaada ya mablanketi 300 kwa
Mwenyekiti wa kijiji cha Lushamba, Deus Bitulo (kulia kwa naibu waziri)
huku Mwenyekiti wa CCM tawi la Nyamango, Japhet Kafula akishuhudia
tukio hilo
Post a Comment