Wakati wa Utawala wa Mwingereza
Baada ya Utawala wa Kijerumani kuanguka na nchi kuchukuliwa na Waingereza mwaka 1920, kwanza nchi ilitumia Noti za Rupee za Afrika ya Mashariki na Rupee za Zanzibar ingawa Rupie za Kijerumani pia ziliendelea kutumika. Kwa upande wa Zanzibar Noti ya Rupee 1 ilianzishwa mwaka 1920. Baadhi ya noti hizo ni hizi hapa:1 Zanzibar Rupee
1 EA Rupee
5 EA Rupee
10 EA Rupee
Katikati ya mwaka 1920, Serikali ya Uingereza ilianzisha sarafu ya pamoja kwa nchi zote za Afrika ya Mashariki iliyojulikana kama Florin ya Afrika ya Mashariki. Noti za Florini zilikuwa katika thamani za Florin 1, 5, 10, 20, 50, 100 na Florin 500, ambapo noti za kuanzia Florin 10 na kuendelea juu zilikuwa pia na thamani ya Pound (1, 2, 5, 10 na 50). Kwa vile sarafu hii haikudumu zaidi ya miezi sita, ni noti chache sana zilizotolewa, mifano ya noti hizo ni kama ifuatavyo:
1 EA Florin
5 EA Florin
Mwanzoni mwa mwak 1921, Serikali ya Kiingereza ilianzisha sarafu ya pamoja Afrika Mashariki iliyojulikana kama Shilingi ya Afrika ya Mashariki na hivyo kuondokana na Florin ya Afrika Mashariki. Shilingi ya Afrika Mashariki (baadaye nitakuwa naandika kwa kifupi tu kama Shilling) ilikuwa na thamani ya Shilingi 20 kwa Pound moja na ilikuwa imeegeshwa kwenye Pound kiasi kuwa thamani ya Shiling 20 kwa Pound haikubadilika (Hii ndiyo sababu Watanzania tuliendelea kuiita shilingi 20 kama 'Pound'). Noti za Shilingi zilizotolewa wakati huo zilikuwa za thamani za Shilingi 5, 10, 20, 100, 1,000, na Shilingi 10,000. Noti za Shilingi ishirini na kuendelea juu zilikuwa pia na thamani ya Pound (1, 5, 50). Noti hizi zilikuwa zimeandikwa kwa Kiingereza, Kiarabu na Kiamhara kinachotumika Ethiopia. Katika utawala wote wa Kiingereza, kulitolewa mitindo miwili tu ya noti hizo. Mtindo wa kwanza ulidumu kuanzia mwaka 1921 hadi mwaka 1958, ma mtindo wa pili ulidumu kuanzia mwaka 1958 hadi baada ya Uhuru mwaka 1964. Sura ya mbele ya noti zote ilikuwa ikionyesha Mtawala wa Himaya ya Uingereza. Sura ya nyuma kwa upande wa noti za mtindo wa kwanza ilikuwa na simba mmoja wa kiume katika eneo la Mlima Kenya. Noti zilizotolewa mara ya kwanza wakati wa Utawala wa Mfalme George wa Tano (1910-1936) ni kama ifuatavyo:
5 EA Shilling
10 EA Shilling
20 EA Shilling
100 EA Shilling
1,000 EA Shilling
Kwa thamani ya shilingi na uchumi wa watu wakati huo, ni noti chache sana zenye thamani ya Shiling 1,000 na Shilingi 10,000 ziliingia kwenye mzunguko, na sikufanikiwa kupata noti ya Shilingi 10,000. Kwa hiyo ilipofika mwaka 1933, serikali ikaamua kusimaisha matumizi ya noti za Shilingi 1,000 ingawa zile za Shilingi 10,000 ziliendelea. Wakati wa utawala mfupi wa Mfalme Edward wa Nane mwaka 1936, hazikutolewa noti zozote. Noti nyingine zilitolewa wakati wa utawala wa Mfame George wa Sita (1936-1952), ambapo noti ya Shilingi 1 ilianzishwa. Noti hizo zilikuwa kama ifuatavyo.
1 EA Shilling
5 EA Shilling
10 EA Shilling
20 EA Shilling
100 EA Shilling
Kutokana na uadimu wake, sikuweza kupata noti za Shilingi 10,000. Hata hivyo miaka 11 ndani ya utawala wa Mfalme George wa Sita, iliamuliwa kufuta noti hizi za Shilingi 10,000 ambazo zilikuwa hazitumiki sana.
Baada ya kifo cha Mfalme George wa Sita mwaka 1952 na binti yake Malkia Elizabeth wa Pili kuchukua usukani noti zilizotolewa zilikuwa zinafanana na zile zilizokuwapo mwanzoni isipokuwa aliondoa noti ya Shilingi 1 kwenye mzunguko.
5 EA Shilling
10 EA Shilling
20 EA Shilling
100 EA Shilling
Mwishoni mwa Utawala wa Kiingereza
Hata hivyo, mwaka 1958, noti hizo zilitengezwa upya katika mtindo tofauti na zile zilizokuwapo mwanzo. Noti mpya zilikuwa na rangi nyingi huku zikionyesha mazao mbali mbali ya uchumi yaliyokuwepo Afrika ya Mashariki. Noti ya Shilingi 5 ilionyesha pamba na karafuu; noti ya Shilingi 10 ilionyesha mkonge na chai; noti ya Shilingi 20 ilionyesha kahawa na alizeti, na mwisho noti ya Shilingi 100 ilionyesha minazi, miwese na pareto. Inaelekea kuwa kuanzia hapo, shilingi ya Afrika Mashariki iliacha kubebeshwa kwenye pound kwa vile noti mpya hazikuwa na thamani ya pound tena.5 EA Shilling
10 EA Shilling
20 EA Shilling
100 EA Shilling
Noti hizi ziliendelea hadi baada ya Uhuru ingawa mwaka 1961 zilifanyiwa marekebsihao madogo kwenye sura ya mbele ili kuweza kuonyesha sahihi sita za Wajumbe wa Bodi ya Fedha ya Afrika Mashariki ambapo wakati huo walikuwa wameongezeka na kuwa sita kutoka watano waliokuwepo mwaka 1958. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:
5 EA Shilling
10 EA Shilling
20 EA Shilling
100 EA Shilling
Baada ya nchi zote za Afrika ya Mashariki kuwa huru, noti za kwanza zilizotolewa mwaka 1964 zilifanyiwa mabadiliko makubwa sana. Kwanza, noti hizi zilikuwa zimeandikwa katika Kiingereza, Kiarabu na Kishwahili; halafu sura ya Mtawala wa Uingereza iliondolewa na badala yake kuwekwa mashua. Sikuweza kufahamu mara moja kwa nini waliamua kutumia mashua. Sura za nyuma za noti ziliendelea kuonyesha mazao mbalimbali ya Afrika ya Mashariki ingawa kwa mpangilio tofauti kama ionekanavyo katika picha hizi.
5 EA Shilling
10 EA Shilling
20 EA Shilling
100 EA Shilling
Utawala wa Nyerere
Utawala wa Mwinyi
Utawala wa Mkapa na Kuendelea Hadi Leo
Wakati Mkapa alipochukua usukani wa kuongoza nchi mwaka 1995, aliamua kusitisha matumizi ya sura za viongozi kwenye noti (kwa kuwa yeye hakutaka iwekwe sura yake, kama alivyokataa kuitwa 'mtukufu rais' bali 'mheshimiwa rais'). Kwa hiyo noti zote zilizotolewa mwaka 1997 chini ya utawala wake hazikuwa na sura ya kiongozi yeyote. Badala yake zilikuwa na kichwa cha Twiga ambaye kihistoria ndiye Mnyama wa Taifa. Wakati huo pia, noti za Shilingi 50, 100 na Shilingi 200 zilisimamishwa.500 Tz Shilling
1000 Tz Shilling
5000 Tz Shilling
10000 Tz Shilling
Hata hivyo, baada ya kifo cha Mwalimu Nyerere mwaka 1999, iliamuliwa kuwa sura yake iwe ya kudumu kwenye noti ya Shilingi 1,000, hivyo noti hiyo ilisanifiwa upya na kuwa kama ifuatavyo:
1000 Tz Shilling
Noti hizi ziliendelea kutumika hadi mwaka 2003 zilipofanyiwa mabadiliko ya kuongeza usalama zaidi. Vile vile kutokana na manung'uniko ya kichinichini kutokea Zanzibar kuhusiana na mtumizi ya Twiga ambaye alikuwa mnyama wa Tanganyika, iliamuliwa kutotumia twiga tena. Badala yake sura za wanyama wakubwa mbalimbali wa Tanzania zilitumika ingawa sura ya Nyerere iliendelea kubaki kwenye noti za Shilingi 1,000. Vile vile noti mpya ya Shilingi 2,000 ilianzishwa. Upande wa nyuma wa noti hizi ulionyesha shughuli mbalimbali za uchumi, sehemu za kihistoria na harakati za kukuza elimu. Kwa mara nyingine tena kuanzia mwaka 1978, noti hizi ziliandikwa kwa Kiingereza na Kishwahili tena. Noti hizi ndizo zinazotumika hadi leo, sura zake ni kama ifuatavyo:
500 Tz Shilling
1000 Tz Shilling
2000 Tz Shilling
5000 Tz Shilling
10000 Tz Shilling
Hatujui mabadiliko yajayo yatakuwaje hasa ikizingatiwa kwamba Shilingi yetu imeendelea kuporomoka thamani kila mwaka. Tusubiri na tuone.
Post a Comment