Abate mstaafu wa Abasia ya Peramiho Jimbo kuu katoliki la Songea Lambert
Doerr OSB katikati wa kati akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa
Waumini wa Parokia ya Mbingamharule Wilayani Songea Mkoani Ruvuma,kama
sehemu ya kumpongeza baada ya kutimiza miaka 50 ya Umisionari hapa
Nchini.
Waumini wa Parokia ya Mbingamharule Jimbo kuu katoliki la Songea
mkoani Ruvuma,wakifuatilia kwa makini adhimisho la misa Takatifu ya
shukurani ya kutimiza miaka 50 ya Umisionari ya Abate mstaafu wa Abasia
ya Peramiho LambeDoerr hapa Nchini.(PICHA NA JULIUS KONALA)
-----------------
Na Julius Konala wa demasho.com,Songea
BAADHI
ya Wasomi mkoani Ruvuma,wamemtaja Abate mstaafu Lambert Doerr OSB wa
Abasia ya Peramiho kuwa ni Mwanahistoria wa karne ya 21 kutokana na
mchango wake mkubwa wa kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo hapa
Nchini ikiwemo katika nyanja ya Elimu.
Matamko
hayo yalitolewa na Wasomi hao kwa nyakati tofauti wakati walipokuwa
wakitoa mada mbalimbali katika kongamano lililoandaliwa kwa ajili ya
kuzungumzia juu ya maisha na kazi zilizofanywa na Abate huyo katika
kipindi chake cha miaka 50 ya Umisionari hapa Nchini
lililofanyika kwenye ukumbi wa Nyerere chuo kikuu cha Sauti tawi la
Songea.
Akitoa
mada katika kongamano hilo Padre Dr.Xsaver Komba,alisema kuwa moja ya
mchango wa uliotolewa na Abate Lambert wakati akiwa Mwalimu bora na
mwadilifu katika
Seminari ndogo ya Likonde na Seminari kuu ya Peramiho alifundisha
kwabidii kwa kufuata misingi ya ualimu iliyopelekea kutoa wasomi wengi
ambao miongoni mwao ni viongozi wakubwa wa Serikali na Dini.
Alisema
kuwa michango mingine aliyoitoa ni pamoja kuwaunganisha Waafrika kuwa
kitu kimoja na wazungu kwenye nyumba za kitawa, kuwasomesha baadhi ya
wananchi wa kijiji cha Mbinga Mharule kwa kuwalipia ada ya
shule,kusogeza huduma ya maji safi na salama kwa kilometa saba,kujenga
zahanati,ujenzi wa barabara ya Lambert yenye urefu wa kilometa
tatu,kusaidia wazee
wasiojiweza,watoto Yatima pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya dini
ya kikristu na waislamu.
Alisema
kuwa maadhimisho hayo ya Jubilei ya miaka 50 ya Umisionari Nchini
yatakwenda sambamba na na uanzishwaji wa chuo cha ufundi cha Mtakatifu
Lambert mjini hapa kitakachotoa fani ya kompyuta,ushonaji na uselemala
kama sehemu ya kumuenzi.
Naye
mmoja wa watoa mada na mwanafunzi aliyefundishwa na Abate
huyo,Dr.Damas Mbogoro ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali hapa
Nchini alimwelezea Abate Lambert kuwa ni mtu ambaye hakuwa mchoyo wa
elimu na kudai kwamba alikuwa karibu na watu katika kusikiliza shida na
matatizo yao.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika kongamano hilo,Padre Dastan Mbano ambaye alimwakilisha Askofu mkuu wa jimbo kuu
katoliki la Songea
Damian Dallu,alisema kuwa Abate Lambert ni hazina kubwa sio kwa upande wa kanisa peke yake bali ni kwa jamii nzima.
Mbano
alisema kuwa kazi nzuri na kumbukumbu za Abate huyo zinapaswa
kutangazwa,kuenziwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya faida ya vizazi vijavyo
huku mwakilishi wa Baraza la mila kasian Shauritanga,alisema kuwa
wamisionari Wabenediktini wa Abasia ya Peramiho watakumbukwa kwa mchango
wao wa kusaidia kutunza kumbukumbu za mila na desturi za wangoni katika
makumbusho ya vita ya majimaji na kuupatia mkoa na taifa kwa ujumla
sifa pekee ya utunzaji.
Post a Comment