Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewahamisha askari wake, WP 5863 Quine na WP 3548 Koplo Maeda kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Ilala kwa kukiuka maadili ya kazi.
Taarifa ya ndani ya Oktoba 2, mwaka huu ya Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu Dar es Salaam iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, imesema askari hao walisimamisha gari dogo na baada ya dereva kujitetea, waliendelea kutafuta makosa hali iliyosababisha abiria aliyekuwa mgonjwa kufariki.
Kutokana na tukio hilo, makamanda wa polisi wa wilaya zote za Mkoa wa Kipolisi wa Dar es Salaam wametakiwa kuwakumbusha askari wao kuepuka kutolazimisha kutafuta makosa ambayo hayana madhara.
“Makosa ambayo hayana madhara katika kusababisha ajali mfano ni vifaa vya kuzimia moto, rangi, kadi kutoandika anuani, motor vehicle, leseni chini ya siku 30 na kadhalika,” lilisomeka agizo hilo kwa makamanda hao wa polisi.
Post a Comment