Baadhi ya washabiki na wapambe wa wakiwa na vipeperushi vilivyotengenezwa maalum kumshangilia Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu mara baada ya kutangazwa
Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa pili,Lillian Kamazima (kulia) na Mshindi wa Tatu,Jihhan Dimachk mara baada ya kutawazwa rasmi usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.Sitti Mtemvu alianza kwa kunyakua Redds Miss Chang'ombe na baadaye Redds Miss Temeke. Sitti ni binti wa Mbunge wa Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu.
Mbunge wa
Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu akizungumza jambo mbele ya wanahabari mara baada ya mtoto wake kutangazwa kuwa
Redd's Miss Tanzania 2014
Redd's Miss Tanzania 2014
Mrembo
wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas akivalishwa taji.
Pichani
ni Washiriki waliochaguliwa kuingia kwenye hatua ya tano bora katika
shindano la Redds Miss Tanzania 2014 linaloendelea hivi sasa ndani ya
ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar.Picha zote na Othman Michuzi.
Mmoja wa Washiriki waliongia katika nafasi ya tanno bora shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakijibu maswali mbalimbali
Mmoja
wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya pichani kulia Ommy Dimpoz
akitumbuiza jukwaani akiwa sambamba na msanii Vanessa Mdee mbele ya
wageni waalikwa (hawapo pichani),waliofika kushuhudia shindano hilo.
Washiriki wa Redds Miss Tanzania 2014 wapatao 15 mara baada ya kuchujwa.
Sehemu
ya baadahi ya Wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye
shindano hilo la kumsaka Kinara wa Redds Miss Tanzania 2014
Baadhi
ya Washiriki wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakicheza moja ya
onesho lao la ufunguzi wa shindano hilo,ambapo mshindi atatangazwa usiku
huu na kujinyakulia kiasi cha shilingi miloni 18 taslim.
Baadhi ya Washiriki wa shindano la Redds Miss Tanzania 2014,wakiwa jukwaani na mavazi ya ufukweni.
Msaniii
wa Muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee a.k.a V-Money akitumbuiza kwenye
shindano la kumsaka mshindi wa Redds Miss Tanzania 2014,yanayofanyika
usiku huu ndani ya moja ya ukumbi wa Mlimani,jijini Dar.
Washiriki wa shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakikatiza jukwaani na mavazi yao ya ubunifu
Baadhi ya Majaji wakifuatilia kwa makini
Pichani
ni Washiriki wa Redds Miss Tanzania 2014 wapatao 30 wakiwa jukwaani
tayari kwa kuanza kuchujwa kupata washiriki 15 bora. Picha zote na Othman
Michuzi.
Siti, binti wa Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu, usiku wa kuamkia jana ameibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania (Redd’s Miss Tanzania 2014) katika shindano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Mlimbwende huyo, ambaye kabla ya kutwaa taji hilo alitawazwa kuwa Miss Temeke, aliwabwaga warembo wengine 30 waliokuwa wakiwania taji hilo mwaka huu.
Kwa ushindi huo, Siti amejinyakulia kitita cha Shilingi milioni 18, ambapo ukumbini hapo alikabidhiwa hundi ya thamani ya Shilingi milioni 10 kwa maelezo kwamba kiasi kilichobaki cha Shilingi milioni 8 atakabidhiwa baada ya shindano hilo.
Siti ataiwakilisha Tanzania kwenye shindano la Miss World mwakani, ambapo mwaka huu Tanzania itawakilishwa na mshindi wa mwaka jana, Happiness Watimanywa kutoka Dodoma.
Post a Comment